Monday, 5 December 2011

MATUKIO MUHIMU MKOA WA KAGERA KIPINDI CHA MIAKA HAMSINI


 
Mwaka 1961
•  Uhuru wa Tanganyika : tarehe 09 Desemba 1961 Mkoa wa Kagera uliungana na mikoa mingine kusherehekea kupatikana kwa Uhuru. Sherehe hizo zilifanyika katika Uwanja wa Uhuru uliopo katika Manispaa ya Bukoba. Uwanja huo ulipewa jina hilo la Uhuru kwa kuwa ndio uliotumika kufanyia mikutano ya kisiasa katika harakati za kudai Uhuru. Maadhimisho makubwa yalifanyika kitaifa mkoani Dar es Salaamna mkoa uliwakilishwa na watu wanne ambao ni Ndugu Samweli Luangisa (Assistant Province Commissioner), Mzee Ziadi alikuwa Mwenyekiti wa TANU, ndugu Abdul Sued Kagasheki aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba na Ndugu Masabala aliwakilisha umoja wa vijana wa TANU.
Mwaka 1962
•  Mafuriko : Mvua kubwa ilinyesha na mafuriko kutokea sehemu kubwa ya Mkoa, ambapo wananchi waliipa jina la “Mvua ya Uhuru” kwa sababu mvua kubwa ya masika ilinyesha baada ya Tanganyika kupata Uhuru.
Mwaka 1963
•  TANICA Yaanzishwa : Kampuni ya Kukoboa Kahawa ya TANICA ilianzishwa. Kampuni hii imechangia kukua kwa pato la mwananchi wa mkoa wa Kagera. Tangu kuanzishwa kwake hadi sasa kampuni hii imetoa ajira nyingi sana kwa wakazi wa mkoa wa Kagera.
•  Kufutwa kwa Tawala za Kichifu (Kitemi) : Tawala za kichifu za Ntare, Nyarubanja, Ruhinda na Rumanyika zilifutwa kutoka na serikali kufuta mfumo huo wa utawala kote nchini.
Mwaka 1965
•  Kuanzishwa kwa Mkoa wa Kagera: Mkoa wa Ziwa Magharibi ambao sasa ni “Kagera” ulianzishwa.
•  Uchaguzi Mkuu : Uchaguzi Mkuu ulifanyika ambapo ulihusisha watemi na Wakama. Watemi na Wakama waliotawala kuanzia mwaka 1965-1970 katika Mkoa wa Kagera ni wafuatao:
•  Bakampenja - alitawala sehemu ya Ihangiro;
•  Kaneno - aliongoza sehemu ya Karagwe;
•  Kasusura – aliongoza sehemu ya Biharamulo;
•  Kasano - aliongoza sehemu ya Kiziba na Missenyi;
•  J. Kibogoyo – aliongoza sehemu ya Kiyanja; na
•  Kami – aliongoza sehemu ya Bugabo na Kyamutwara.
Orodha ya Wabunge tangu Uhuru ipo kuanzia Kiambatanisho Na 4.
Mwaka 1966
•  Ukame : Ukame mkubwa uliodumu hadi mwaka 1970 watokea na kusababisha njaa kali katika wilaya ya Karagwe. Hali hiyo ilisababisha baadhi ya watu kupoteza maisha, kupungua kwa nguvukazi, baadhi ya familia kukosa matunzo kwa ukaribu baada ya wanaume kwenda maeneo ya mbali kutafuta chakula.
Mwaka 1970
•  Uchaguzi Mkuu : Uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge ulifanyika katika majimbo matano ya Uchaguzi ya Biharamulo, Bukoba, Karagwe, Muleba na Ngara. Waliochaguliwa kuwakilisha majimbo hayo ni Ndugu Kasusura (Biharamulo), Ndugu Ishungisa (Karagwe), Ndugu Zimbihire (Muleba) na Ndugu Niboye (Ngara). Kwa Wilaya ya Bukoba ambayo ilikuwa kubwa na ilikuwa ikiendeleza utawala wa watemi na wakama, iliwakilishwa na wawakilishi watatu kwa kupigiwa kura na wananchi wa Wilaya hiyo. Waliowakilisha wilaya hiyo walikuwa Ndugu Kibogoyo, Ndugu Kasano na Ndugu Rutagwerela.
Mwaka 1972
•  Machafuko ya mpakani: Matatizo katika mpaka wa Tanzania na Uganda (Kaskazini mwa Mto Kagera) matatizo haya yalisababisha kutokea kwa vita ya muda mfupi kati ya Tanzania na Uganda ambayo baadaye tatizo hili lilimalizwa kwa suluhisho la nchi hizi mbili.
Mwaka 1975
•  Kuanzishwa kwa Wilaya ya Muleba : Wilaya ya Muleba ilianzishwa kwa kuunganisha Tarafa ya Ihangiro, Kimwani na baadhi ya kata za Tarafa ya Kihanja.
Mwaka 1976
•  Kuanzishwa kwa kijiji cha Kyamnyorwa katika wilaya ya Muleba kutokana na operesheni ya vijiji. Katika kijiji cha Kyamyorwa kulikua na ardhi yenye rutuba, na huduma nyingine muhimu kama maji. karibu na huduma stahili ambapo waliishi kwa pamoja na kufanya kazi kwa pamoja na miongoni mwa vijiji bora.
Mwaka 1977
•  Kuanzishwa kwa Chama cha Mapinduzi : sherehe za kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi zilifanyika mkaoni kwenye uwanja wa uhuru.
Mwaka 1978
•  Vita kati ya Tanzania na Uganda : Mwezi Oktoba 1978 kulitokea vita kati ya nchi ya Tanzania na nchi ya Uganda . Vita hii ilijulikana kwa jina maarufu la “vita ya Kagera” iliitwa jina hilo kutokana kwamba ilipiganiwa katika ardhi ya Tanzania mkoani Kagera.
Vita hii ilisababishwa na kitendo cha Majeshi ya Uganda, chini ya Nduli Idd Amin Dada, kuvamia ardhi ya Tanzania katika eneo la Missenyi na kudai kuwa eneo lote lililo kaskazini mwa Mto Kagera ni ardhi ya nchi ya Uganda. Vita hivyo vilimalizika mwezi April, 1979 kwa Majeshi ya Tanzania kushinda vita na kumuondoa madarakani Nduli Idd Amin.
Vita hivi vya Kagera vilikuwa na athari kubwa kwa mkoa wa Kagera. Athari hizo ni pamoja na vifo, wananchi kunyang'anywa mali zao na uharibifu wa miundombinu ya majengo na barabara.
Mwaka 1979
  Mkoa wa Ziwa Magharibi wabadilishwa Jina : Baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda Mkoa wa Ziwa Magharibi ( West Lake ) ulibadilishwa jina na kuitwa Kagera.
•  Uwanja wa Uhuru wabadilishwa Jina: Uwanja wa Uhuru uliopo mjini Bukoba ambao ulitumika mwaka 1961 kusherehekea Uhuru ulibadilishwa jina na kuitwa “Uwanja wa Jenerali Mayunga” kwa kumbukumbu ya vita ya Kagera na heshima ya shujaa na kiongozi wa vita hivyo.
Mwaka 1983
•  Operesheni Uhujumu Uchumi : Kutokana na kukosekana kwa bidhaa muhimu katika jamii na kupungua kwa uwianao wa kipato kati ya walio nacho na wasio nacho serikali iliendesha operesheni dhidi ya wahujumu uchumi nchi nzima. Wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera walitupa bidhaa zao kwenye Ziwa Victoria na mto Ngono ili kuhofia kukamatwa na Serikali.
 
•  Kugunduliwa kwa Mgonjwa wa UKIMWI: Ugonjwa unadhoofisha kinga za mwili za kujikinga na maradhi, ambao baadae ulikuja kujulikana zaidi kama UKIMWI (Ukosefu wa Kinga Mwilini), uligundulika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mkoani Kagera. Ugonjwa huu uligunduliwa katika hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ya Ndolage iliyoko wilaya ya Muleba ambapo mgojwa wa kwanza aliyegundulika kuwa na virusi vya UKIMWI alitoka katika Kijijini cha Kanyigo Wilaya ya Missenyi.Hospitali ya Ndolage ilikuwa ya kwanza kutoa huduma ya kupima UKIMWI katika mkoa wa Kagera.
Mwanzoni wananchi wa Mkoa wa Kagera waliuita ugonjwa huo “ Juliana” au “Slim”. Uliitwa Julianakwa sababu iliaminika kuwa ugonjwa huo uliingizwa nchini na vijana waliokuwa wakitokea Uganda wakiwa wamevaa mashati ya Juliana. Pia uliitwa ‘slim' kwa sababu waathirika wa ugonjwa huo walikuwa wanakonda hadi kufa. Ugonjwa huu baadae ulienea Tanzania nzima na kuleta athari kubwa katika jamii. Mkoa wa Kagera ulikuwa wa kwanza kuathirika. Ugonjwa huu uliwakumba zaidi vijana, wanajamii ambao wanaotegemewa sana katika uzalishaji mali . Vijana wengi wakaangamia kwa UKIMWI na kufanya familia nyingi kubaki na wazee wakibeba mzigo wa kutunza watoto yatima. Pia muda mwingi wa kuzalisha mali ulipotea katika kuhudhuria mazishi na matanga ya ndugu na jamaa, kuuguza wagonjwa na kutunza yatima. Ugonjwa wa UKIMWI bado upo mpaka sasa katika mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla ambapo kiwango cha maambukizi mkoani Kagera ni asilimia 3.4.
Mwaka 1985
•  Uchaguzi Mkuu: Uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu, na Tanzania ilipata Rais wa awamu ya pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.
Mwaka 1990
•  KDCU na KCU Vyaanzishwa: Chama Kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Karagwe na Chama Kikuu cha Ushirika cha Kagera (KCU) vyaanishwa.
Mwaka 1992
•  Mfumo wa Vyama Vingi: Mfumo wa vyama vingi vya siasa waanzishwa nchini na kuingia mkoani Kagera kwa kufunguliwa matawi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), United Democratic Party (UDP), NCCR-Mageuzi, United Movement for Democracy (UMD) na Tanzania Labour Party (TLP).
Mwaka 1994
•  Kuingia kwa Wakimbizi wa Rwanda na Burundi : Kutokana na mapigano ya kikabila nchini Burundi na mauaji ya kimbari nchini Rwanda , inakadiriwa kuwa Wanyarandwa na Warundi 750,000 waliingia mkoani Kagera wakikimbia mapigano hayo. Ujio wa wakimbizi ulisababisha madhara makubwa kwa mkoa wa Kagera yakiwemo uharibifu wa mazingira na kushamili kwa uhalifu mwingiliano wa utamaduni, kuzaliana Hadi kufikia Juni, 2011 wakimbizi wote walikuwa wamerudi katika nchi zao.
•  Kuanguka kwa ndege: Ajali ya kuanguka kwa ndege ya Jeshi yasababisha vifo na majeruhi kwa abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo
Mwaka 1995
•  Mvua kubwa: Mvua kubwa ilinyesha na kusababisha mafuriko na uharibifu wa mazao na miundombinu. Mafuriko yaliathiri sana Wilaya yote ya Bukoba na Missenyi. Madaraja yalisombwa na maji hivyo kuathiri watumiaji na baadhi ya nyumba za watu ziliharibiwa.
•  Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa Vyama Vingi : Kutokana na kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 uchaguzi mkuu ulifanyika ukihusisha vyma vingi. V yama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi huo mkoani Kagera ni Chama cha Mapinduzi (CCM), United Democratic Party (UDP), NCCR-Mageuzi, United Movement for Democracy (UMD) na Tanzania Labour Party (TLP).
Mwaka 1996
•  Kuzama kwa MV Bukoba: MV Bukoba ikiwa safirini kutoka Bukoba kwenda Mwanza, ilizama katika Ziwa Victoria kilomita nane kabla ya kufika bandari ya Mwanza. Inakadiriwa kuwa watu mia nane (800, kati yao watu wapatao 580 wakikadiriwa kutoka Mkoa wa Kagera). Aidha mali yenye thamani ya mamilioni ya shilingi ilipotea. Sababu za kuzama kwa meli hiyo kulisababishwa na ujazaji wa abiria na miziko kupita uwezo wake.
Kiasi cha shilingi 294.4 kilitolewa na Serikali kwa Mkoa wa Kagera, ikiwa ni rambirambi kwa wafiwa na pole kwa walionusurika.
Mwaka 1997
•  Mradi wa KAEMP waanzishwa: Katika kukabiliana na athari za wakimbizi, mkoani Kagera mradi mkubwa wa Kilimo na Usimamizi wa Mazingira, uliojukana zaidi kwa jina la KAEMP ( Kagera Agricultural and Environmental Management Program ) ulianzishwa. Programu hii ilileta mapinduzi makubwa katika maendeleo ya kilimo, mazingira, afya, maji na barabara.
•  Mvua za El – Nino: Mvua kubwa za El Nino zilinyesha na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu ya wakazi wa Kagera hasa barabara na madaraja. Aidha, nyumba na mali mbalimbali za wananchi ziliharibiwa hivyo wananchi kuhitaji msaada wa Serikali.
Mwaka 2000
•  Uchaguzi Mkuu : Uchaguzi mkuu wa pili katika mfumo wa vyama vingi wafanyika huku kukiwa na ongezeko la majimbo ya uchaguzi. Majimbo hayo mapya yalitokana na kugawanywa kwa Jimbo la Muleba na kuwa na majimbo ya Muleba Kaskazini na Muleba Kusini na kugawanywa ka Jimbo la Biharamulo na majimbo ya Biharamulo Mashariki na Biharamulo Magharibi. Jimbo la Bukoba pia liligawanywa na kuwa na majimbo ya Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini na Nkenge. Jimbo la Karagwe nalo liligawanywa na kuwa majimbo ya Karagwe na Kyerwa.
Mwaka 2002
•  Benki ya Wakulima (KFCB) Yaanzishwa: Benki ya wakulima ambayo inamilikiwa na kusimamiwa na vyama vya ushirika vya msingi, vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa, mfuko wa mazao na chama kikuu cha ushirika KCU ilianzishwa. Makao makuu ya benki hii yapo Manispaa ya Bukoba
•  Oparesheni maalum ya kusaka majambazi: Oparasheni hii ilihusisha vikosi mbalimbali vya Jeshi kutoka Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Mgambo pamoja na Idara ya Usalama wa Taifa. Idara ya Wanyamapori nayo ilihusika katika zoezi hili. Kwa ujumla zoezi hili lilikuwa na mafanikio makubwa
Mwaka 2004
•  Kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru: Mwenge wa Uhuru wawashwa kwenye uwanja wa Kaitaba na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Ali Mohamed Shein tarehe 07 Juni 2004 na kukimbizwa katika Wilaya zote za mkoa wa Kagera na baadaye kukabidhiwa Mkoa wa Kigoma.
Mwaka 2006
•  Kuanzishwa kwa Wilaya ya Chato: Wilaya ya Chato yaanzishwa kwa kuigawa Wilaya ya Biharamulo. Eneo la wilaya mpya ya Chato ni eneo lote la liliokuwa Jimbo la Uchaguzi la Biharamulo Mashariki likiwa na Tarafa 3, Kata 14 na Vijiji 74. Bw. Said Mkumbo ndiye alikuwa mkuu wa wilaya wa kwanza wa wilaya hiyo.
•  Kuanzishwa kwa Wilaya ya Missenyi: Wilaya ya Missenyi yaanzishwa kwa kuigawa Wilaya ya Bukoba. Wilaya ya Missenyi ina ukubwa wa hekta 270,875, na inaundwa na tarafa 2, kata 20, vijiji 74 na vitongoji 350. Ina jimbo moja la uchaguzi liitwalo Nkenge, madiwani 20 wa kuchaguliwa na 8 viti maalum. Bw. Elias Maarugu ndiye alikuwa mkuu wa wilaya wa kwanza wa wilaya hiyo.
Mwaka 2007
•  Kagera Day : Kagera Day Fund Rising” ilifanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 27 Novemba 2007 ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maendeleo ya elimu mkoani Kagera. Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Fedha zilizopatikana zilisaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara na ununuzi wa bati. Madarasa matatu yalijengwe katika shule ya sekondari za Ijuganyondo (mjini Bukoba) na madarasa matatu pia katika shule ya Sekondari Bugene (iliyopo wilayani Karagwe).
Aidha, maabara yalijengwa katika shule sita za Kagondo (Muleba), Shyunga (Ngara), Rubondo (Biharamulo), Makurugusi (Chato), Izimbya (Bukoba Vijijini) na Bunazi (Missenyi).
Jumla ya bati 600 zilinunuliwa na kugawanywa bati 75 kwa kila Halmashauri.
Mfuko wa Kagera Day umeweza pia kupata wafadhili ambao wameleta kompyuta 51 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari.
Mwaka 2009
•  Mafuriko Chato: Mvua kubwa yanyesha wilayani Chato na kusababisha mafuriko makubwa yaliyoharibu mazao mashambani na miundombinu mbalimbali.
 

IDARA YA ELIMU MKOANI KAGERA

 
Dira ya Sekta ya Elimu kama ilivyobainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inaelekeza ufanisi na utoaji wa elimu kwa lengo la kumuwezesha kila Mtanzania kuwa na ujuzi wa Stadi za kuinua hali yake ya kiuchumi pamoja na kushiriki kikamilifu katika Maendeleo ya Taifa. Mkoa wa Kagera umeendelea kusimamia na kutekeleza dira hiyo kwa lengo la kuboresha elimu katika ngazi zote kama inavyofafanuliwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995.
 
 
ELIMU YA AWALI
Sera ya elimu ni kila shule ya msingi kuwa na darasa la awali. Madarasa ya awali yameongezeka kutoka 692 (mwaka 2005) hadi madarasa 1008 (mwaka 2011) sawa na ongezeko la 46%.
Kati ya shule 1,008 zenye madarasa ya awali, shule 960 ni za serikali na shule 48 ni za watu binafsi /Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Shule za awali zina jumla ya wanafunzi 73,264 (Was. 36,346 na Wav 36,918) ambao wamegawanyika kiwilaya/halmashauri kama ifuatavyo:
IDADI YA SHULE ZA AWALI NA WANAFUNZI KI-WILAYA MWAKA 2011
WILAYA
SHULE ZA AWALI
WANAFUNZI
 
 
 
SERIKALI
 
BINAFSI
 
JUMLA
 
WAS
 
WAV
Biharamulo
84
5
89
2,682
2,623
5,305
Chato
125
2
127
4,574
4,715
9,289
Bukoba (V)
141
5
146
4,719
4,745
9,464
Missenyi
95
5
100
2,816
2,959
5,775
Bukoba (M)
20
12
32
1,048
1,181
2,229
Karagwe
200
6
206
8,628
8,790
17,418
Muleba
185
8
193
6,148
6,065
12,213
Ngara
110
5
115
5,731
5,840
11,571
JUMLA
960
48
1,008
36,346
36,918
73,264
 
MIKAKATI YA KUBORESHA ELIMU YA AWALI
• Mwamko wa Elimu katika jamii kuwa mdogo na muda mwingi kutumika katika uhamasishaji na ufuatiliaji.
•  Kipato duni kwenye familia – jambo linalopelekea uandikishaji usiende kwa wakati ama mzazi kushindwa kumpeleka mtoto shuleni kwa kisingizio kwamba fedha ya kumpatia mtoto ili anunue mahitaji ya msingi kama sare, michango ya uji/uendeshaji kituo cha awali.
•  Umbali mrefu kutoka kwenye jamii hadi shule ilipo husababisha wazazi kushindwa kuwaandikisha watoto mwenye umri unaotakiwa kwa kuhofia kuwa hawawezi kuhimili umbali huo.
•  Uyatima – Baadhi ya watoto wanashindwa kuandikishwa kwa wakati kutokana na kufariki kwa wazazi wao. Fedha ya ruzuku inayotolewa inawalenga wanafunzi wa shule ya msingi na Elimu ya Awali hawahusishwi kabisa.
•  Madarasa wanayotumia wanafunzi wa Elimu ya Awali ni ya shule za msingi hivyo hufanya kuwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi darasani.
•  Shule nyingi za awali hazina vifaa na zana za kufundishia na kujifunzia mfano:- Mipira, Bembea, Vipandio, Ringi, jezi na kadi.
•  Shule za awali zina walimu wachache wenye vyeti vya elimu awali.
•  Wazazi hawana wito wa kuchangia huduma za elimu awali.
 
ELIMU YA MSINGI
Mkoa wa Kagera unatambua kwamba elimu ni ufunguo wa maisha na kwamba maendeleo ya sekta nyingine yana uhusiano wa karibu na maendeleo ya elimu hivyo Sekta ya Elimu imepewa kipaumbele. Katika kutekeleza dhima hii ya taifa mkoa wa Kagera umeweka mkazo katika kuboresha elimu kwa kuzingatia mambo muhimu ambayo ni pamoja na:-
•  Upatikanaji wa walimu
•  Ujenzi wa vituo vya mafunzo vya Walimu (Teachers Resource Centres)
•  Uandikishaji wa watoto wa kuingia darasa la kwanza
•  Ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za Walimu
•  Ujenzi wa vyoo katika Shule .
 
 
 
Idadi ya Shule za Msingi na Wanafunzi
Mkoa una jumla ya shule za Msingi zipatazo 1,050 zenye wanafunzi 533,987. kati ya hizo shule 1,003 ni za serikali na shule 47 zinamilikiwa na mashirika mbalimbali au watu binafsi. Mchanganuo wa shule hizo kwa kila halmashauri ni kama ulivyoainishwa:-
H/MASHAURI
SHULE
WANAFUNZI
SERIKALI
BINAFSI
JUMLA
WAS
WAV
JUMLA
BIHARAMULO
85
2
87
20,686
21,502
42,188
CHATO
126
2
128
40,092
39,951
79,286
BUKOBA (V)
141
5
146
39,335
32,835
66,060
MISSENYI
95
5
100
33,225
20,306
40,461
BUKOBA(M)
23
12
35
10,464
10,112
20,576
MULEBA
221
8
229
50,964
50,615
101,579
KARAGWE
202
9
211
56,276
59,900
116,176
NGARA
110
4
114
34,343
33,318
67,661
JUMLA
1,003
47
1,050
270,438
268,539
533,987
MIKAKATI
Mkoa wa Kagera umejizatiti kuboresha Elimu kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali katika utekelezaji wa mambo ya msingi kwa kutumia mikakati ifuatayo :-
  • Kuzishauri halmashauri kuendelea na ujenzi wa majengo ya shule ili kila shule iweze kuwa na mikondo minne.
  • Kuhamasisha wazazi na wananchi kwa ujumla kuhusu uhimizaji wa mahudhurio na ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi shuleni.
  • Kuhakikisha taarifa za shule zinazotolewa na wakaguzi wa shule zinafanyiwa kazi ili kuondoa mapungufu yaliyoainishwa.
  • Kuhakikisha kuwa wazazi wenye watoto wa umri wa kwenda shule wanaandikishwa mapema.
  • Kuendeleza mafunzo ya ufundi katika vyuo vilivyopo ili kujenga ujasiriamali miongoni mwa vijana wanaohitimu mafunzo hayo.
  • Kuzishauri halmashauri kuwaendeleza walimu kwa kuwapeleka katika mafunzo ya muda mfupi na mrefu ili kupata maarifa mapya yanayoletwa kupitia utandawazi.
Kuhimiza halmashauri kujenga moyo wa uchangiaji maendeleo ya elimu miongoni mwa wananchi ili kuinua ubora wa elimu.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Shule ya Sekondari ya kike ya Rugambwa mkoani Kagera
 
Idadi ya Walimu Katika Shule za Msingi – Hadi Oktoba 2011
Mkoa wa Kagera unahitaji jumla ya walimu 15,299 ili kukidhi kiwango kilichowekwa cha uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 40. Idadi ya walimu hadi mwezi Juni 2011 ilikuwa walimu 9,896 sawa na 65% ya mahitaji. Idadi hii ni sawa na uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 54. Mchanganuo wa mahitaji na walimu waliopo kwa kila halmashauri ni kama ifuatavyo:-
IDADI YA WALIMU, MAHITAJI, WALIOPO NA UPUNGUFU HADI
JUNI 2011
WILAYA
MAHITAJI
WALIOPO
UPUNGUFU
UWIANO
Biharamulo
1,128
768
360
1:61
Bukoba (M)
499
483
6
1:43
Bukoba “V'
1,621
1,351
270
1:49
Karagwe
4,048
1,962
2,086
1:60
Muleba
2,499
1,885
614
1:54
Ngara
2,132
1,282
850
1:53
Chato
2,441
1,309
1,132
1:61
Missenyi
931
846
85
1:49
JUMLA
15,299
9,896
5,403
1:54

ELIMU YA SEKONDARI

Elimu ya Sekondari
Mkoa wa Kagera una jumla ya shule 240. kati ya hizo shule 204 ni za Serikali na 36 zinamilikiwa na mashirika au watu binafsi. Mchanganuo wa shule zilizopo kwa kila halmashauri ni ma ifuatavyo.
SHULE ZA SEKONDARI HADI MWAKA 2011
NA
WILAYA
SERIKALI
BINAFSI
 
JUMLA
1.
BIHARAMULO
18
2
20
2.
BUKOBA (M)
19
7
26
3.
BUKOBA (V)
30
5
35
4.
CHATO
17
-
17
5.
KARAGWE
38
9
47
6.
MISSENYI
19
3
22
7.
MULEBA
35
6
41
8.
NGARA
22
4
26
JUMLA
204
36
240
Mkoa pia umeweza kufungua/kupanua shule 6 mwaka 2010 ambazo zinapokea wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita. Shule hizo ni Jikomboe na Magufuli (Chato), Kagango, Biharamulo na Nyakahura (Biharamulo) na Rutabo iliyoko Muleba.
Sekretarieti ya mkoa katika inaendelea kuzihimiza halmashauri kuwa na shule angalau moja yenye wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita ili kuongeza idadi ya wanafunzi katika kiwango hiki cha elimu.
Mimba Mashuleni
Katika kipindi cha Januari 2009 hadi Desemba 2011 jumla ya wanafunzi waliopata mimba ni 133. Kati ya hao wanafunzi wa shule za msingi ni 41 na wa shule za sekondari ni 92. Halmashauri zimechukua hatua mbalimbali dhidi ya watu waliosababisha ujauzito kwa wanafunzi hawa. Baadhi ya kesi zipo mahakamani, polisi na zingine ziko kwenye uongozi wa kata. Mchanganuo wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa kila halmashauri ni kama inavyoonyeshwa
IDADI YA WANAFUNZI WALIOPATA MIMBA KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUANZIA JANUARI 2009 HADI SEPTEMBA 2011
NA
HALMASHAURI
MSINGI
SEKONDARI
JUMLA
1
BIHARAMULO
1
12
13
2
BUKOBA MANISPAA
-
2
2
3
BUKOBA VIJIJINI
-
13
13
4
CHATO
5
21
26
5
KARAGWE
13
16
29
6
MISSENYI
5
3
8
7
MULEBA
17
9
26
8
NGARA
-
17
17
JUMLA
41
92
133
ELIMU YA WATU WAZIMA
MEMKWA
Mpango wa Elimu ya Msingi Kwa Walioikosa (MEMKWA) ulianzishwa ili kuwasaidia wanafunzi waliokuwa wamepita umri wa kwenda shule kuweza kupata fursa ya kujifunza.
•  Halmashauri za Wilaya ya Ngara na Bukoba Vijijini ndizo zilikuwa za kwanza kuanza kutekeleza mpango huu.
•  Halmashauri za Muleba, Biharamulo, Manispaa ya Bukoba na Karagwe zilianza kutekeleza mpango huu mwaka 2005.
•  Jumla ya wanafunzi 9,963 sawa na asilimia 47 ya wanafunzi 20,967 waliotarajiwa wameweza kuandikishwa chini ya mpango huu hadi mwaka 2007. Jumla ya wawezeshaji ni 721.
Halmashauri zinahimizwa ili kuhakikisha kuwa matarajio waliyoweka yanafikiwa. Hali ya uandikshaji ni nzuri kwa manispaa ya Bukoba na Chato. Jitihada za makusudi zinahitajika kwa Halmashauri zilizosalia.
ELIMU YA UFUNDI
Mkoa una jumla ya vyuo vya Ufundi 31. kati ya hivyo vyuo vya Serikali ni 5 na 26 ni vya Taasisi au watu binafsi. Jumla ya wanachuo katika vyuo hivi ni 675 wakiwemo wanawake 315 na wanaume 360.
Fani zinazofundishwa katika vyuo hivi ni pamoja na Useremala, Uashi, Sayansi Kimu, TEHAMA, Ushonaji na Uhunzi.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikana na wizara nyingine imeunda kamati ya kukarabati na kuanzisha vyuo vya Ufundi katika halmashauri zisizo na vyuo hivi.
 
 
 

USTAWI WA JAMII MKOANI KAGERA

USTAWI WA JAMII
Mkoa wa Kagera kama ilivyo mikoa mingine yaTanzania unaendelea kutoa huduma za ustawi wa jamii kwa wananchi wake. Watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi wanaendelea kuongezeka siku hadi siku kwenye Mkoa wa kagera.
Sababu zinazopelekea kuongezeka kwa watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi ni pamoja na:- Vifo vya akina mama baada ya kujifungua, Magonjwa ya akili kwa mama akiwa na mtoto mchanga, magonjwa hasa janga la UKIMWi, Mifarakano ya familia na uteketezaji wa watoto kutokana na hali ngumu ya maisha.
Aidha Kwa kipindi cha mwaka 2010/2011, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali (mashirika ya dini, taasisi zisizo za kiserikali pamoja na watu binafsi) Mkoa unaendelea kutoa huduma za Ustawi wa Jamii katika maeneo yafuatayo:-
 
Kutoa huduma kwa makundi maalum
•  Watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi
•  Watu wenye ulemavu
•  Wazee
 
Huduma kwa Watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi
Mkoa una jumla ya watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi 85,594 ambao wamebainishwa katika Halmashauri za Mkoa wa Kagera. Mkoa kwa kushirikiana na taasisi za dini na mashirika ya yasiyo ya serikali unatoa huduma kwa watoto wapatao 46,376, kati yao wanawake ni 23,038 na wanaume ni 23,338.
Idadi ya watoto waliotambuliwa na Halmashuri wanazotoka imeoneshwa kwenye jedwali hapo chini:
S/N
HALMASHAURI
ME
KE
JUMLA
1.
Ngara
3,118
3,062
6180
2.
Misenyi
4,585
4,671
9256
3.
Karagwe
3,515
3,415
6,930
4.
Bukoba Manispaa
844
1,105
1,949
5.
Muleba
12,905
12,455
25,360
6.
Chato
7,600
7,252
14,852
7.
Bukoba
9,021
8,210
17,231
8.
Biharamulo
2,055
1,781
3,836
 
JUMLA
43,643
41,951
85,594
Misaada iliyotolewa ni pamoja na karo za shule, sare za shule, vyakula, nguo, sabuni matandiko ya nyumbani pamoja na matumizi mengine. Pamoja na kuwajengea nyumba za kuishi mifugo mbalimbali hutolewa kwa walengwa kwa ajili ya kujiongezea kipato na kujikwamua na umasikini. Huduma nyingine ni kutoa elimu juu ya janga la UKIMWI, unafundisha staid za kazi na kilimo bora kwa kuzingatia sera ya “kilimo Kwanza ”. Baada ya kuwapatia elimu hiyo vijana pamoja na walezi wao wanapewa mbegu bora za mazao mbalimbali kwa ajili ya uzalishaji.
Taasisi na mashirika yanayotoa huduma ni TADEPA, MAPEC, WAMATA, KARADEA, SAWAKA, WOMEDA, WvT, HUYAWA Roman Catholic, Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania, Humuliza, Matumaini Mapya, PACT Tanzania, UNICEF kupitia Global Fund na mashirika mengi yaliyopo hapa Mkoani
Mkoa una jumla ya vitua na makao 16, vituo 11 ni makao ya watoto yatima, vituo 2 watoto wa mitaani, 1 ni makao ya wazee, na 2 ni makao ya walemavu. Kati ya hivyo vituo 3 vinaendeshwa na Serikali, 7 mashirika ya dini na vituo 6 vinavyoendeshwa watu binafsi.
Huduma kwa wazee
Mkoa una kituo kimoja cha kutunza wazee ambacho kiko chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii. Kituo kina jumla ya wazee 17 kati yao wanawake 7 na wanaume 10 .
Mkoa unatoa huduma ya matibabu bure kwa wazee kwenye kila kituo cha kutolea huduma za afya.
Huduma kwa familia zenye matatizo
Huduma iliyotolewa ni pamoja na ushauri nasaha, kupewa matibabu na kulipiwa bima za afya, na kutembelea familia ili kutoa ushauri katika familia husika.
Kipindi cha Julai 2010 hadi Juni 2011 Mkoa umepokea jumla ya mashauri 24 ya ya ndoa, mashauri 31 ya matunzo nje ya ndoa mashauri 1 ya kunyang'anywa watoto. Mashauri hayo yalishughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi na wahusika waliridhika na utatuzi huo isipokua mashauri saba ya ndoa, na mashauri 3 ya kunyang'anywa watoto yalipelekwa mahakamani ili kutolewa uwamuzi wa kisheria.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Bi. Rebbeca Gwambasa----Afisa Ustawi wa Jamii-Mkoa wa Kagera
Huduma kwa watu wenye ulemavu
Mkoa umehakikisha kwamba jamii ya watu wenye ulemavu wanalindwa na kupewa haki ya kuishi kama raia wengine, Mkoa umezitaka Halmashauri na Serikali za vijiji kuhakikisha kwamba walemavu wote, hasa wa ngozi (Albino) wanalindwa na kuhifadhiwa dhidi ya wauaji
Idadi ya walemavu waliotambuliwa na Halmashuri wanazotoka imeoneshwa kwenye jedwali hapo chini:
S/N
HALMASHAURI
ME
KE
JUMLA
1.
Bukoba Manispaa
269
253
522
2.
Muleba
130
300
430
3.
Missenyi
215
500
715
4.
Bukoba Vijijini
125
300
425
5.
Chato
-
-
-
6.
Ngara
233
650
883
7.
Biharamulo
303
325
628
8.
Karagwe
420
520
940
 
JUMLA
1695
2848
4543
Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa ambayo ilikumbwa na wimbi la mauaji na mashambulizi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) tatizo la mashambulizi na mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa Mkoa wa Kagera lilijitokeza mwezi septemba mwaka 2008. wilaya ambazo tatizo hili lilijitokeza ni Ngara, Biharamulo Muleba na Karagwe. Mkoa ulipoteza watu wenye ulemavu wa ngozi wapatao 5 na mmoja alikatwa viungo vya mwili wake na kuwa kilema wa maisha, sababu kubwa zilizojitokeza kuhusiana na tatizo hili ni imani potopfu ya baadhi ya watu ambao wanaamini kuwa viungo vya binadamu wenye ulemavu wa ngozi vinasaidia kupata utajiri.
Mkoa ulifanya jitihada ya kuwaelimishwa kuhusu kuwalinda walemavu wa ngozi kuachana na imani za kishirikina zinazosababisha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, na kila kijiji kimeagizwa kuwatunza albino waishio katika vijiji vyao.
MAFANIKIO
•  Mkoa umefanikiwa kutoa huduma za matibabu bure kwa wazee wanaofika hospitali mbalimbali hasa Hospitali ya mkoa na hospitali za Wilaya.
•  Kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Walemavu, Mkoa wa Kagera umefanikiwa kuunzisha Mfuko wa watu wenye ulemavu (Walemavu Trust Fund) ili kuwasaidia walemavu kuendesha shughuli mbalimbali.
•  Mkoa umefanukiwa kuwaweka pamoja watoto walemavu wa ngozi (Albino) kwenye shule ya msingi ya Mugeza mseto kwa ajili ya usalama wao, pamoja na kupatiwa elimu kama watoto wengine.
•  Kuimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali na mashirika ya dini katika kutoa huduma mbalimbali kwa makundi maalum.
CHANGAMOTO ZINAZOKABILI SEKTA YA USTAWI WA JAMII
  • kwa kuwa makundi hayo yanaongezeka kwa kasi kwenye jamii yetu, Hakuna takwimu sahihi za walemavu, wazee, watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.
  • Jamii haijapata mwamko katika kuchangia fedha katika mifuko ya kusaidia watoto walio katika mazingira magumu.
  • Uwezo mdogo na umasikini unasababisha wazazi/walezi kutelekeza familia zao kwa sababu wanashindwa kuzihudumia.
  • Hakuna ufadhili endelevu hivyo kusababisha baadhi ya viyuo kukosa mahitaji muhimu kwa ajili ya watoto.
 
MIKAKATI YA KUKABILI CHANGAMOTO HIZI:-
•  Kutambua watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, walemavu na wazee ili kupata takwimu sahihi kwa kuwa makundi hayo yanaongezeka kila siku kwenye jamii yetu.
•  Kutayarisha maeneo yatakayotumika kutoa huduma za afya kwenye vituo vyote vinavyotoa huduma ya afya na kuwa na watoa huduma kwa ajili ya kwa wazee.
•  Kuhamasisha Jamii juu ya kutambua umuhimu wa kuchangia mfuko wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
•  Kushauri wananchi kuunda vikundi ili wapate mafunzo ya ujasiriamali kusudi waweze kujikwamua katika umasikini.
•  Kuelimisha jamii kuondokana na mila potofu zinazopelekea mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino), yatokanayo na imani potofu za utafutajimali.