Dira ya Sekta ya Elimu kama ilivyobainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inaelekeza ufanisi na utoaji wa elimu kwa lengo la kumuwezesha kila Mtanzania kuwa na ujuzi wa Stadi za kuinua hali yake ya kiuchumi pamoja na kushiriki kikamilifu katika Maendeleo ya Taifa. Mkoa wa Kagera umeendelea kusimamia na kutekeleza dira hiyo kwa lengo la kuboresha elimu katika ngazi zote kama inavyofafanuliwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995. |
ELIMU YA AWALI Sera ya elimu ni kila shule ya msingi kuwa na darasa la awali. Madarasa ya awali yameongezeka kutoka 692 (mwaka 2005) hadi madarasa 1008 (mwaka 2011) sawa na ongezeko la 46%. Kati ya shule 1,008 zenye madarasa ya awali, shule 960 ni za serikali na shule 48 ni za watu binafsi /Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Shule za awali zina jumla ya wanafunzi 73,264 (Was. 36,346 na Wav 36,918) ambao wamegawanyika kiwilaya/halmashauri kama ifuatavyo: IDADI YA SHULE ZA AWALI NA WANAFUNZI KI-WILAYA MWAKA 2011
WILAYA | SHULE ZA AWALI | WANAFUNZI |
| SERIKALI | BINAFSI | JUMLA | WAS | WAV |
Biharamulo | 84 | 5 | 89 | 2,682 | 2,623 | 5,305 |
Chato | 125 | 2 | 127 | 4,574 | 4,715 | 9,289 |
Bukoba (V) | 141 | 5 | 146 | 4,719 | 4,745 | 9,464 |
Missenyi | 95 | 5 | 100 | 2,816 | 2,959 | 5,775 |
Bukoba (M) | 20 | 12 | 32 | 1,048 | 1,181 | 2,229 |
Karagwe | 200 | 6 | 206 | 8,628 | 8,790 | 17,418 |
Muleba | 185 | 8 | 193 | 6,148 | 6,065 | 12,213 |
Ngara | 110 | 5 | 115 | 5,731 | 5,840 | 11,571 |
JUMLA | 960 | 48 | 1,008 | 36,346 | 36,918 | 73,264 |
|
MIKAKATI YA KUBORESHA ELIMU YA AWALI • Mwamko wa Elimu katika jamii kuwa mdogo na muda mwingi kutumika katika uhamasishaji na ufuatiliaji. • Kipato duni kwenye familia – jambo linalopelekea uandikishaji usiende kwa wakati ama mzazi kushindwa kumpeleka mtoto shuleni kwa kisingizio kwamba fedha ya kumpatia mtoto ili anunue mahitaji ya msingi kama sare, michango ya uji/uendeshaji kituo cha awali. • Umbali mrefu kutoka kwenye jamii hadi shule ilipo husababisha wazazi kushindwa kuwaandikisha watoto mwenye umri unaotakiwa kwa kuhofia kuwa hawawezi kuhimili umbali huo. • Uyatima – Baadhi ya watoto wanashindwa kuandikishwa kwa wakati kutokana na kufariki kwa wazazi wao. Fedha ya ruzuku inayotolewa inawalenga wanafunzi wa shule ya msingi na Elimu ya Awali hawahusishwi kabisa. • Madarasa wanayotumia wanafunzi wa Elimu ya Awali ni ya shule za msingi hivyo hufanya kuwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi darasani. • Shule nyingi za awali hazina vifaa na zana za kufundishia na kujifunzia mfano:- Mipira, Bembea, Vipandio, Ringi, jezi na kadi. • Shule za awali zina walimu wachache wenye vyeti vya elimu awali. • Wazazi hawana wito wa kuchangia huduma za elimu awali. |
ELIMU YA MSINGI |
Mkoa wa Kagera unatambua kwamba elimu ni ufunguo wa maisha na kwamba maendeleo ya sekta nyingine yana uhusiano wa karibu na maendeleo ya elimu hivyo Sekta ya Elimu imepewa kipaumbele. Katika kutekeleza dhima hii ya taifa mkoa wa Kagera umeweka mkazo katika kuboresha elimu kwa kuzingatia mambo muhimu ambayo ni pamoja na:- • Upatikanaji wa walimu • Ujenzi wa vituo vya mafunzo vya Walimu (Teachers Resource Centres) • Uandikishaji wa watoto wa kuingia darasa la kwanza • Ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za Walimu • Ujenzi wa vyoo katika Shule . |
| |
Idadi ya Shule za Msingi na Wanafunzi Mkoa una jumla ya shule za Msingi zipatazo 1,050 zenye wanafunzi 533,987. kati ya hizo shule 1,003 ni za serikali na shule 47 zinamilikiwa na mashirika mbalimbali au watu binafsi. Mchanganuo wa shule hizo kwa kila halmashauri ni kama ulivyoainishwa:-
H/MASHAURI | SHULE | WANAFUNZI |
| SERIKALI | BINAFSI | JUMLA | WAS | WAV | JUMLA |
BIHARAMULO | 85 | 2 | 87 | 20,686 | 21,502 | 42,188 |
CHATO | 126 | 2 | 128 | 40,092 | 39,951 | 79,286 |
BUKOBA (V) | 141 | 5 | 146 | 39,335 | 32,835 | 66,060 |
MISSENYI | 95 | 5 | 100 | 33,225 | 20,306 | 40,461 |
BUKOBA(M) | 23 | 12 | 35 | 10,464 | 10,112 | 20,576 |
MULEBA | 221 | 8 | 229 | 50,964 | 50,615 | 101,579 |
KARAGWE | 202 | 9 | 211 | 56,276 | 59,900 | 116,176 |
NGARA | 110 | 4 | 114 | 34,343 | 33,318 | 67,661 |
JUMLA | 1,003 | 47 | 1,050 | 270,438 | 268,539 | 533,987 |
MIKAKATI Mkoa wa Kagera umejizatiti kuboresha Elimu kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali katika utekelezaji wa mambo ya msingi kwa kutumia mikakati ifuatayo :- - Kuzishauri halmashauri kuendelea na ujenzi wa majengo ya shule ili kila shule iweze kuwa na mikondo minne.
- Kuhamasisha wazazi na wananchi kwa ujumla kuhusu uhimizaji wa mahudhurio na ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi shuleni.
- Kuhakikisha taarifa za shule zinazotolewa na wakaguzi wa shule zinafanyiwa kazi ili kuondoa mapungufu yaliyoainishwa.
- Kuhakikisha kuwa wazazi wenye watoto wa umri wa kwenda shule wanaandikishwa mapema.
- Kuendeleza mafunzo ya ufundi katika vyuo vilivyopo ili kujenga ujasiriamali miongoni mwa vijana wanaohitimu mafunzo hayo.
- Kuzishauri halmashauri kuwaendeleza walimu kwa kuwapeleka katika mafunzo ya muda mfupi na mrefu ili kupata maarifa mapya yanayoletwa kupitia utandawazi.
Kuhimiza halmashauri kujenga moyo wa uchangiaji maendeleo ya elimu miongoni mwa wananchi ili kuinua ubora wa elimu.
|
|
| |
|
|
| |
|
| |
| |
|
| |
| |
| |
|
| |
|
| |
| |
| |
| |
| |
|
| |
| |
| |
| |
| |
![]() |
| Shule ya Sekondari ya kike ya Rugambwa mkoani Kagera |
Idadi ya Walimu Katika Shule za Msingi – Hadi Oktoba 2011 Mkoa wa Kagera unahitaji jumla ya walimu 15,299 ili kukidhi kiwango kilichowekwa cha uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 40. Idadi ya walimu hadi mwezi Juni 2011 ilikuwa walimu 9,896 sawa na 65% ya mahitaji. Idadi hii ni sawa na uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 54. Mchanganuo wa mahitaji na walimu waliopo kwa kila halmashauri ni kama ifuatavyo:- IDADI YA WALIMU, MAHITAJI, WALIOPO NA UPUNGUFU HADI JUNI 2011
WILAYA | MAHITAJI | WALIOPO | UPUNGUFU | UWIANO |
Biharamulo | 1,128 | 768 | 360 | 1:61 |
Bukoba (M) | 499 | 483 | 6 | 1:43 |
Bukoba “V' | 1,621 | 1,351 | 270 | 1:49 |
Karagwe | 4,048 | 1,962 | 2,086 | 1:60 |
Muleba | 2,499 | 1,885 | 614 | 1:54 |
Ngara | 2,132 | 1,282 | 850 | 1:53 |
Chato | 2,441 | 1,309 | 1,132 | 1:61 |
Missenyi | 931 | 846 | 85 | 1:49 |
JUMLA | 15,299 | 9,896 | 5,403 | 1:54 |
ELIMU YA SEKONDARIElimu ya Sekondari Mkoa wa Kagera una jumla ya shule 240. kati ya hizo shule 204 ni za Serikali na 36 zinamilikiwa na mashirika au watu binafsi. Mchanganuo wa shule zilizopo kwa kila halmashauri ni ma ifuatavyo. SHULE ZA SEKONDARI HADI MWAKA 2011
NA | WILAYA | SERIKALI | BINAFSI | JUMLA |
1. | BIHARAMULO | 18 | 2 | 20 |
2. | BUKOBA (M) | 19 | 7 | 26 |
3. | BUKOBA (V) | 30 | 5 | 35 |
4. | CHATO | 17 | - | 17 |
5. | KARAGWE | 38 | 9 | 47 |
6. | MISSENYI | 19 | 3 | 22 |
7. | MULEBA | 35 | 6 | 41 |
8. | NGARA | 22 | 4 | 26 |
JUMLA | 204 | 36 | 240 |
Mkoa pia umeweza kufungua/kupanua shule 6 mwaka 2010 ambazo zinapokea wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita. Shule hizo ni Jikomboe na Magufuli (Chato), Kagango, Biharamulo na Nyakahura (Biharamulo) na Rutabo iliyoko Muleba. Sekretarieti ya mkoa katika inaendelea kuzihimiza halmashauri kuwa na shule angalau moja yenye wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita ili kuongeza idadi ya wanafunzi katika kiwango hiki cha elimu. Mimba Mashuleni Katika kipindi cha Januari 2009 hadi Desemba 2011 jumla ya wanafunzi waliopata mimba ni 133. Kati ya hao wanafunzi wa shule za msingi ni 41 na wa shule za sekondari ni 92. Halmashauri zimechukua hatua mbalimbali dhidi ya watu waliosababisha ujauzito kwa wanafunzi hawa. Baadhi ya kesi zipo mahakamani, polisi na zingine ziko kwenye uongozi wa kata. Mchanganuo wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa kila halmashauri ni kama inavyoonyeshwa IDADI YA WANAFUNZI WALIOPATA MIMBA KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUANZIA JANUARI 2009 HADI SEPTEMBA 2011
NA | HALMASHAURI | MSINGI | SEKONDARI | JUMLA |
1 | BIHARAMULO | 1 | 12 | 13 |
2 | BUKOBA MANISPAA | - | 2 | 2 |
3 | BUKOBA VIJIJINI | - | 13 | 13 |
4 | CHATO | 5 | 21 | 26 |
5 | KARAGWE | 13 | 16 | 29 |
6 | MISSENYI | 5 | 3 | 8 |
7 | MULEBA | 17 | 9 | 26 |
8 | NGARA | - | 17 | 17 |
JUMLA | 41 | 92 | 133 |
ELIMU YA WATU WAZIMA MEMKWA Mpango wa Elimu ya Msingi Kwa Walioikosa (MEMKWA) ulianzishwa ili kuwasaidia wanafunzi waliokuwa wamepita umri wa kwenda shule kuweza kupata fursa ya kujifunza. • Halmashauri za Wilaya ya Ngara na Bukoba Vijijini ndizo zilikuwa za kwanza kuanza kutekeleza mpango huu. • Halmashauri za Muleba, Biharamulo, Manispaa ya Bukoba na Karagwe zilianza kutekeleza mpango huu mwaka 2005. • Jumla ya wanafunzi 9,963 sawa na asilimia 47 ya wanafunzi 20,967 waliotarajiwa wameweza kuandikishwa chini ya mpango huu hadi mwaka 2007. Jumla ya wawezeshaji ni 721. Halmashauri zinahimizwa ili kuhakikisha kuwa matarajio waliyoweka yanafikiwa. Hali ya uandikshaji ni nzuri kwa manispaa ya Bukoba na Chato. Jitihada za makusudi zinahitajika kwa Halmashauri zilizosalia. ELIMU YA UFUNDI Mkoa una jumla ya vyuo vya Ufundi 31. kati ya hivyo vyuo vya Serikali ni 5 na 26 ni vya Taasisi au watu binafsi. Jumla ya wanachuo katika vyuo hivi ni 675 wakiwemo wanawake 315 na wanaume 360. Fani zinazofundishwa katika vyuo hivi ni pamoja na Useremala, Uashi, Sayansi Kimu, TEHAMA, Ushonaji na Uhunzi. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikana na wizara nyingine imeunda kamati ya kukarabati na kuanzisha vyuo vya Ufundi katika halmashauri zisizo na vyuo hivi. |
| |
|
|
|
No comments:
Post a Comment