Friday, 4 November 2011

RISALA YA UZINDUZI WA MIAKA HAMSINI (50) YA UHURU WILAYANI KARAGWE TAREHE 04/11/2011 /20

1.UTANGULIZI.
Mh.Mgeni Rasmi,
Ninachukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwako kwa kukubali wito wakuungana nasi katika sherehe hii ya uzinduzi wa Miaka Hamsini (50)ya Uhuru Wilayani Karagwe sambamba na Sikukuuu ya Wakulima Nane Nane Mwaka 2011.
 
1.1 HALI YA WILAYA KWA UFUPI
Wilaya ya Karagwe ni kati ya Wilaya 8 za Mkoa wa Kagera .inapatikana katika Latitude nyuzi 1º hadi 20º Kusini ya Ikweta na Longitude 30º hadi 38º. 30” Mashariki mwaGreenwich . Wilaya inapakana na Nchi ya Uganda upande wa Kaskazini, Nchi ya Rwandaupande wa Magharibi, Wilaya ya Ngara upande wa Kusini na Wilaya ya Misenyi na Mleba upande wa Mashariki. Mto wa Kagera upo mpakani mwa Wilaya ya Karagwe na Nchi ya Rwanda na sehemu ya Kaskazini Magharibi mwa Nchi ya Uganda .
 
Wilaya ina eneo la Kilimita za Mraba 7,716,kati ya hizo Kilomita za Mraba 7,558 ni eneo la nchi kavu na Kilomita za Mraba 158 ni eneo la maji. Mwinuko wa Ardhi kutoka usawa wa Bahari ni Mita 1500 hadi Mita 1800. mwinuko mrefu ni Mlima wa Rwabunuka .Hali ya hewa kwa ujumla ni joto la wastani wa 20- 26ºC. Mvua zinanyesha kwa wastani wa Milimita 1,040 hadi 1,200 kwa Mwaka kati ya Mwezi September na Januari na kati ya Mwezi Machi na Mei.
 
1.2  UTAWALA
Kiutawala Wilaya imegawanyika katika Tarafa 9, Kata 40 Vijiji 166 na Vitongoji 1,373. Katika mgawanyiko huu, Tarafa 5 Kata 12 Vijiji 57 na Vitongoji 211 ni vipya. Tangu Mwezi Julai 2010 Serikali iliridhia ombi la kuanzisha Wilaya mpya ya Kyerwa, iliyo na Tarafa 4 Kata 18, Vijiji 93 na jumla ya Vitongoji 646. Tunayo majimbo 2 ya uchaguzi ya Karagwe na Kyerwa yaliyo na Wabunge wafuatao:-
- Jimbo la Karagwe- Mhe.Gosbert Blandes (CCM)
- Jimbo la Kyerwa- Mhe. Eustace.O.Katagira(CCM)
 
 
 
 
1.3  IDADI YA WATU
Kwa mjibu wa Sensa ya Mwaka 2002 Wilaya ilikuwa na watu 423,423.
(Me 207,850 na Ke 215,573). Ongezeko la watu kwa Mwaka ni Asilimia 2.9. Hivyo inakadiliwa kwa kutumia ongezeko hilo Mwaka 2011 Wilaya ilikuwa na idadi ya watu wapatao 639,651.
 
2. HISTORIA YA WILAYA
Wilaya ya Karagwe ilizinduliwa Mwaka 1958 na Gavana Richard Turnbull baada ya kumegwa kutoka katika Wilaya ya Bukoba. Kwa hali hiyo Wilaya ya Karagwe ilikuwepo wakati Tanganyika inapata Uhuru wake hapo tarehe 9/12/1961. Wakati huo shughuli za kiutawala zilikuwa zinafanyika katika maeneo mawili tofauti yahani Kayanga na Nyakahanga (yaani Ahalukiko). Baadae Kayanga ikawa ndiyo Makao Makuu ya kiutawala ambako Mkuu wa Wilaya alikuwa akifanya kazi wakati huo Nyakahanga palikuwa panatumiwa na Omkama kama Makao Makuu yake.
 
Kabla ya Uhuru kulikuwa na utawala wa Ma-chifu (Omukama) na Mabaraza yaliyojulikana kama Gombolola. Chifu (Omukama ) alisaidiwa na Katikiro ambaye alikuwa msaidizi wake Mkuu. Chini ya uongozi wa Katikiro walikuwepo wasaidizi waliojulikana kama Abakungu. Kazi ya Abakungu ilikuwa ni kuhakikisha amani na usalama vinakuwepo kusimamia na kuhimiza maendeleo na kutoza kodi ya kichwa.
 
MUUNDO WA WILAYA WAKATI WA UHURU NA JINSI ULIVYOBADILIKA
Wakati wilaya inaanza waka 1958 ikuwa imegawanyika katika maeneo ya utawala yaliyokuwa yanajulikana kama “subchiefs”. Haya maeneo yalikuwa 7 nayo ni
Bugene – palijulikana kama migongo
Nyaishozi – palijulikana kama kiyanja
Nyabiyonza – palijulikana kama chikuba
Kituntu – palijulikana kama bugabwe
Mabira – palijulikana kama marungu
Kaisho – palijulikana kama buganga (karagwe keifo)
Murongo- palijulikana kama buganga
 
Kila “subchief” ilikuwa na kiongozi wake aliyefahamika kama mwami wa gombolola ambaye alifanya kazi chini ya chifu (omukama wa karagwe).
 
Mwaka 1965, “subchiefs” hizo ambazo baadae zilikuja kuitwa kata zilizoongezwa na kuwa 28 hadi mwaka 2010 nazo ni bugene ihanda nyakahanga kiruruma bweranyange kibondonyakakika  kayanga ndama rugu nyakasimbi ihembe nyaishozi nyabiyonza kihanga kituntu igurwa mabira kimuri kamuri rwabwere nkenda kaisho isingiro murongo kyerwa kibingo na  bugomora.
 
Watu wenye uhalifu mdogo na wenye kesi za migogoro ya ardhi walikuwa wanahukumiwa kwenye “subchiefs” hizo. Wenye kuhusika na mauaji na kesi za mogogoro ya ardhi walipelekwa bukoba ambapo omukama alihukumu kesi/mashauri yaliyowashinda abakungu.
 
Na pia ziliundwa tarafa 4 ambazo ni
Bugene/nyaishozi
Nyabiyonza
Kutuntu/mabira
Kaisho/murongo
Baada ya baraza kuvunjwa na machifu  kuondolewa,wilaya ilipata  mkuu wa  wilaya  wa kwanza  mwananchi  aliyeitwa  ndugu  Peter Kafanabo  mwaka  1961.Pia alikuwa katibu wa  kwanza wa  TANU Karagwe.
 
Halmashauri  ya  wilaya  ya  Karagwe ilaundwa  mwaka  1965 wakati  huo  ikiwa inajulikana kama  Buhaya district council hadi mwaka 1872 chni ya uenyekiti wa ndugu Ferdinand Mujungu. Baada ya hapo ilivunjwa na kuwa “district development council” hadi mwaka  1984. mwaka 1984 ndipo ilipoundwa Halmashauri hii ilipo sasa. Tangu  wakati huo wenyeviti wake wamekuwa kama ifuatayo:-                                                                                                                 
     
       1.ndugu H.N Kyakatuka                   1984-1988.
       2.ndugu Salvatory Kalabamu           1989-2005.
      3.ndugu S.R kashunju                        2006-mpaka sasa.
     
    Pia wakurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe tangu ianzishewe mwaka 1984 ni kama ifuatavyo:-
1.Ndugu G.E. KAgaruki                 1984-1986
2.Ndugu E.J. Muganda                   1986-1989
3.Ndugu T.K. Ndibarema                1989-1992     
4.Ndugu O.K. Mwasha                    1992-1998
5.Ndugu S.A Masindike                  1998-2002
6.Ndugu M.S. Mboje                       2002-2006
7.Bibi C.M. Kamuhabwa                 2006-2010
8.Bwana  E Kahabi (Kaimu)            2010 hadi sasa
 
 
HALI YA UONGOZI TANGU 1961
            Wilaya ya Karagwe imewahi kuwa na uongozi wa wakuu wa wilaya kama ifuatavyo:-
1.Marehemu PETER N. KAFANABO            1961-1965
2.Marehemu ENOS RYANGARO                  1965-1969
3.Ndugu LOSA LIYEMBA                              1969-1973
4.Ndugu THOMAS MSONGE                          1973-1977
5.Ndugu RUHASI                                              1977-1978
6.Lt. F.X.ITALA                                               1978-1980
7.Ndugu RAPHAEL CHAYEKA                     1980-1984
8.Marehemu MOHAMED CHAMSALA          1984-1989
9.Ndugu LUHOZYA E.SIWALE                       1984-1989
10.Capt. JOSEPH E. NDITI                                1989-1997
11.Ndugu GERARD J.GHACHOCHA              1997-1999
12.Ndugu PETER KANGWA                             1999-2000
13.Ndugu SANGO OLETELELE                       2000-2004
14.Ndugu DAVID J. DAUD                                2004-2006
15.Ndugu FRANK UHAHULA                           2006-2009
16.Col.Mst FABIAN I.MASSAWE                     2009hadi sasa
              
MATUKIO NA MABADILIKO MAKUU KISIASA, KIUCHUMI, KIUTAWALA, KIULINZI, KITEKNOLOJIA NA KIJAMII.
a)     KISIASA
Wilaya ya karagwe ilianzishwa mwaka 1958 chini ya utawala wa wakoloni. Mabadiliko ya kwanza kisiasa yalikuwa ni yale ya utawala kutoka kwa wakoloni kwenda kwa wananchi wenyewe kupitia uhuru wetu wa mwaka 1961. aidha viguvugu la mfumo wa vyama vingi vya siasa lilianza mapema katika harakati za kutaka kujitawala kutoka kwa wakoloni wa kiingereza na utawala wa kifalme wa kiarabu vyama hivyo ni TANU TAA AFROSHIRAZ PARTY. Baada ya uhuru uongozi wan chi ulikuwa chini ya chama kimoja cha TANU na baadaye CCM. Mabadiliko ya sasa ni utawala wa vyama vyingi vya siasa vilivyosajiliwa ni CCM,CHADEMA,CUF,TLP,na NCCR Mageuzi. Mwenyekiti  wa kwanza wa TANU alikuwa Bwana Kahungya. Waliofuatia tangu wakati huo ni kama ifuatavyo:-
1.     Ndugu Eliakim Kahungya
2.     Ndugu Martin Pancras
3.     Ndugu Fredinand Majungu
4.     Ndugu Hezekiel Kyakatuka
5.     Ndugu Gregory Rwabutomize
6.     Capt.Salvatory Rwechungura
7.     Ndugu Audax Kagaruki
8.     Ndugu Justinian Kazungura 2007 hadi sasa.
 
Aidha Wilaya ya Karagwe iliwahi kuwa na Wabunge wafuatao:-
JINA                                                                     MWAKA                      JIMBO
1.     Mheshimiwa Gervase Kaneno                  1965 – 1968                  Karagwe
2.     Mheshimiwa Laurent Nyamalaba             1968 – 1975                 Karagwe
3.     Mheshimiwa Venant Rwabuti                   1975 – 1980                 Karagwe
4.     Mheshimiwa Elikano Byeitima                  1980 – 1995                Karagwe
5.     Mheshimiwa Sir George Kahama               1995 – 2005                Karagwe
6.     Mheshimiwa Eustace O.Katagira                1995 – 2000               Kyerwa
7.     Mheshimiwa Mtungirehi                              2000 – 2005               Kyerwa
8.     Mheshimiwa Gosbert Blandes                      2005 – hadi sasa       Karagwe
9.     Mheshimiwa Eustace O.Katagira                 2005 – hadi sasa        Kyerwa
 
b)    KIULINZI
Kabla ya kupata uhuru mwaka 1961, ulinzi wilayani karagwe ulikuwa ni ule wa jadi.baadae mgambo, askari polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama viliongezwa. Mwaka 1978/1979 sehemu ya wilaya ya karagwe ilikuwa miongoni mwa maeneo yaliyovamiwa na majeshi ya Uganda sehemu ya mpakani mwa Tanzania na Uganda . Kati ya mwka 1993 na 1994, wilaya ilikumbwa na wimbi la wahamiaji haramu kutoka nchi ya Rwanda ambao walikuwa wanakimbia mauwaji ya kimbari. Wahamiaji haramu haao walifuata njia zilizopitiwa na Ndugu zao mwaka 1957 – 1962 ambao pia walikuwa wanakimbia vita vya kikabila.
 
Athari za matukio haya:-
a)     vita vya kagera iliathiri hali ya maendeleo hasa katika sehemu za mpakani katika kata za mrongo, Bugomora na kibingo.
b)    Wimbi la wahamiaji haramu lilipelekea kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu na uharibifu wa mazingira. Mifugo (ng’ombe) waliibiwa kutoka wilayani kwenda nchi jirani za Uganda na Rwanda kwa wingi maeneo mengi ya karagwe yalianza kukaliwa na wahamiaji haramu. Nafasi za masomo nyingi hasa shule za msingi zilijazwa wahamiaji haramu, hata nafasi za kazi za maofisini na katika sekta ya afya nazo zilijazwa na wahamiaji haramu. Hata baada ya nchi za Uganda na Rwanda kuwa na amani na usalama wimbi kubwa la wafanyakazi waliosomeshwa na taifa hili walihamia katika mataifa yao na kuacha pengo la kiutumishi Tanzania
 
c) KIUTAWALA
Mwaka 2011 mabadiliko makubwa yaliyotokea na serikali kuridhia mgawanyiko wa wilaya kutoka kuwa moja hadi kuwa mbili yaani wilaya ya karagwe  na wilaya ya kyerwa. Aidha mabadiliko yafuatayo yametokea baada ya mgawanyiko wa wilaya ya karagwe.
Tarafa zimeongezeka toka 4 za awali hadi 9 za sasa
-kata zimeongezwa kutoka 28 hadi 40
-vijiji vimeongozwa toka 109 hadi 166
- mamlaka ya mji mdogo wa kayanga imeanzishawa
-waheshimiwa madiwani wa kata mpya walichaguliwa kata uchaguzi mkuu wa mwaka 2011.
 
d)  KIUCHUMI
Mabadiliko makubwa yaliyotokea kuichumi ni pamoja na kupanuka kwa kilimo ambacho ndiyo shughuli kuu ya kiuchumi ya wananchi wa karagwe. Uzalishaji wa kilimo kwa mazao kama ndizi, mahindi, maharage viazi matunda kahawa n.k. umeongezeka kulingana na kipindi nchi yetu inapata uhuru mwaka 1961. aidha kabla ya uhuru madini ya TIN yalikuwa yanachimbwa huko kyerwa. Uchimbaji huo kwa sasa umebakia kwa wachimbaji wadogowadogo tu. Wakati huo umeme wa kutumia nguvu za maji (HEP)ulizalishwa kutoka kwenye maporomoko mya mto kagera eneo la mrongo hadi kyerwa “syndicate” kwa ajili ya kuchimba kusafisha na kubagua TIN. Mitambo hiyo ya umeme iliharibiwa na Idd Amin wakati wa vita vya kagera 1978 – 1979 .
 
Hali ya maaendeleo kiuchumi imekuwa kubwa kwa upande wa kilimo kwani uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara hasa kahawa umeongezeka. Kukua huku wa uchumi kumeenda sambamba na kuongezeka kwa watu hususani wahamiaji kutoka wilaya zingine za bukoba muleba biharamulo na ngara.
 
a)     KITEKNOLOJIA
Wakati Tanganyika inapata uhuru mwaka 1961 hali ya maendeleo ya kiteknolojia wilayani karagwe ilikuwa duni. Kwa sasa hali imekuwa tofauti kuna umeme, kuna mawasiliano ya simu za mezani na mkononi, kuna matumizi ya computer na internet n.k. umeme uliokuwepo kabla ya uhuru ulitoka kikagati  Uganda na kwenda kyerwa kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya bati (TIN). Umeme huo uliondolewa baada ya machimbo hayo kufungwa na matokeo ya vita vya kagera.
b)    KIJAMII
Wakati Tanganyika inapata uhuru, wilaya ilikuwa na huduma chache za kijamii zilizokuwa zikiwafikia watu wachache. Kwa mfano:-
·        Kulikuwa na shule chache sana za msingi lakini pia kulikuwa na shule zilizokuwa zikijulikana kama middle schools nazo ni lukajange nyaishozi bugene rwambaizi shule ya kwanza ya sekondari kuanzishwa wilayani karagwe ilikuwa karagwe sekondari iliyoanzishwa mwaka 1977 na kanisa la kilutheri na ilianzia katika majengo ya rukajange middle school.
·        Kulikuwa na zahanati tatu nyakahanga isingiro na nyakaiga ambazo zote zilikuwa zikimilikiwa na madhehebu ya dini.
·        Mawasiliano ya simu hayakuwepo hususani simu za viganja
·        Umeme ulioenea sehemu kubwa ya wilaya haukuwepo umeme wa sasa uliletwa baada ya vita ya Tanzania na Uganda na hasa katika kipindi cha utawala wa rais Mseveni
·        Huduma ya maji safi na salama iliwafikia watu wachache walioishi mjini kayanga na omurushaka.
 
1.     MAFANIKIO YALIYOPATIKANA TANGU UHURU HADI SASA 
a)     Elimu
 Shule zimeongezeka sana na hadi sasa wilaya ina shule za msingi 212 na sekondari 48. kuna vyuo viwili vya ualimu ambavyo vinaendelea kujengwa na pia kuna mpango wa kujenga chuo kikuu cha kilimo chini ya kanisa la kiinjili la kilutheri .
 
b)    afya
wilaya ina zahanati 50,kati ya hizo 38 ni za serikali na zilizobaki ni za binafsi. Vituo vya afya vipo 5,vinne vya serikali na kimoja cha shirika la dini
 
c)     mtandao wa barabara za wilaya umeimalishwa na kwa sasa una jumla ya km. 518.7,tabaka la lami nyepesi ni km 13 (kutoka mugakorongo hadi nyakahanga Hospital) barabara za tabaka la udongo ni km. 384. barabara kutoka kyaka hadi bugene yenye urefu wa km.59 inajengwa kwa kiwango cha lami hivi sasa.
 
d)    kuna huduma za uhakika za mawasiliano ya simu
 
e)     kuna huduma ya umeme katika baadhi ya maeneo ya wilaya
 
f)      kuna radio za jamii za FADECO na radio karagwe ambazo zimesaidia jamii kupata habari elimu na burudani.
 
g)     Upatikanaji wa mafuta aina zote na vyombo vya usafiri na usafirishaji wa uhakika ambao umewezesha uchumi wa wilaya kukua kwa kasi.
 
h)    Uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara umeongezeka ukilinganisha na watu wa uhuru.
 
2.      
3.     CHANGAMOTO
Wilaya ya karagwe bado inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa kikwazo kwa hatua kubwa zaidi za maendeleo kufikiwa
Changamoto hizi ni pamoja na :-
a)     Wananchi kutokuwa tayari kuchangia miradi ya maendeleo kwa hiari hivyo kukwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani .
b)    Huduma za jamii hazijaweza kuwafikia wananchi kwa kiasi kinachostahili mathalani huduma ya maji afya elimu na kadhalika hivyo jitihada zaidi zinahitajika kurekebisha hali hii.
c)     Mamba za utotoni bado ni tatizo na ni changamoto kubwa inayoikabili wilaya hivyo juhudi zaidi zinafanyika kurekebisha hali hii, kama vile kuwapeleka watuhumiwa katika vyombo vya sheria na kuelimisha jamii.
d)    Uharibifu wa mazingira bado pia ni tatizo hasa uchomaji wa moto misitu hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa kurekebisha hali hii hasa kutoa onyo na elimu kwa wananchi kupitia radio za jamii zilizopo karagwe na kuchukua hatua za kisheria kwa wanaobainika kutenda vitendo vya uharibifu wa mazingira.
e)     Magendo ya kahawa kwenda nchi jirani nayo ni changamoto kwa wilaya. Hatua mbalimbali zimechukuliwa kutatua tatizo hili kubwa zaidi ikiwa ni kuweka ulinzi wa doria kwa kushirikisha uongozi na jamii katika mialo iliyobainila kuwa ndiyo vivuko haramu kuvusha kahawa.
 
4.     MATARAJIO
Matarajio ya wilaya ya karagwe katika kipindi cha miaka 50 ijayo ni kuhakikisha kuwa huduma za jamii kama vile afya elimu maji n.k. inawafikia wananchi wote wa wilaya hii.
-      kuendelea kuimalisha mawasiliano ya simu ili mitandao ya simu za mikononi iweze kiwafikia wananchi wa vijiji vyote.
-      Kuhakikisha kuwa umeme unawafikia wananchi wengi zaidi
-      Kutekeleza mipango ya kilimo ili wananchi wa wilaya hii walime kilimo chenye tija na ufugaji bora wa mifugo ya aina mbalimbali.
-      Kuinua kipato cha wilaya na cha mwananchi mmoja mmoja hasa kupitia kilimo cha mazao ya biashara, chakula na mbogamboga.
-      Kuboresha kilimo cha kahawa kama zao la biashara kwa kuwapa bei nzuri wakulima kuimalisha vyama vya ushirika sambamba na uanzishaji wa SACCOS za wakulima wa kahawa huduma za ugani kudhibiti magendo ya kahawa na kuhamasisha ununuzi binafsi ili kuleta ushindani wa bei.
-      Kuhamasisha wakulima wapande migomba ya kisasa inayostahimili magonjwa ili kuongeza uzalishaji wa ndizi kama zao la biashara na chakula.
 
Naomba kuwasilisha.

Thursday, 3 November 2011

IMPORTANT THINGS ABOUT GADHAFFI

Is this what you call dictator? Is Gaddafi being potrayed correctly?
1. There is no electricity bill in Libya ; electricity is free for all its citizens.
2. There is no interest on loans, banks in Libya are state-owned and loans given to all its citizens at 0% interest by law.
3. Home considered a human right in Libya 4. All newlyweds in Libya receive $60,000 Dinar (US$50,000) by the government to buy their first apartment so to help start up the family.
5. Education and medical treatments are free in Libya . Before Gaddafi only 25% of Libyans are literate. Today the figure is 83%.
6. Should Libyans want to take up farming career, they would receive farming land, a farming house, equipments, seeds and livestock to kick-start their farms – all for free.
7. If Libyans cannot find the education or medical facilities they need in Libya, the government funds them to go abroad for it – not only free but they get US$2,300/mth accommodation and car allowance.
8. In Libyan, if a Libyan buys a car, the government subsidized 50% of the price.
9. The price of petrol in Libya is $0.14 per liter.
10. Libya has no external debt and its reserves amount to $150 billion – now frozen globally.


11. If a Libyan is unable to get employment after graduation the state would pay the average salary of the profession as if he or she is employed until employment is found.
12. A portion of Libyan oil sale is, credited directly to the bank accounts of all Libyan citizens.
13. A mother who gives birth to a child receive US$5,000
14. 40 loaves of bread in Libya costs $ 0.15
15. 25% of Libyans have a university degree
16. Gaddafi carried out the world’s largest irrigation project, known as the Great Man-Made River project, to make water readily available throughout the desert country.Gogele and see this!!!!

UJENZI WA CHUO KIKUU WILAYANI KARAGWE NA JUHUD FELIX

Zaidi ya shilingi milioni 800  zinatakiwa kukamilisha ujenzi wa Chuo Kikuu cha kanisa la Kilutheri Dayosisi ya Karagwe kinachotarajiwa kuanza ujenzi wake Juni mwaka huu.

Hayo yamesemwa jana na mchungaji Daktari Brighton Katabaro ambaye pia ni mratibu wa uanzishwaji wa chuo kikuu Karagwe wakati akisoma taarifa ya azma  na mchakato wa uanzishwaji chuo kikuu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kayanga wilayani hapa.

Daktari Katabaro alisema kuwa ili kukamilisha ujenzi wa chuo kikuu hicho zaidi ya shilingi milioni 800 zinatakiwa ili kusiwepo na kukwama ujenzi utakapoanza  katika kata ya Kihanga  kijiji  cha Kishoju wilayani Karagwe.

Daktari alisema kuwa fedha hizo zitapatikana kutokana na michango mbalimbali ya wananchi ,Taasisi za kiserikali ,na zisizo za kiserikali pamoja na kuchangia kwa njia ya harambee ili kufanikisha azma ya ujenzi wa chuo kikuu.

Alisema kuwa Dayosisi inayo ardhi kubwa na ya kutosha kabisa kwa ujenzi wa chuo kikuu zaidi ya hekta 372 zilizoko katika kijiji cha Kishoju,kuwa dayosisi ya Karagwe inaazimia kuanzisha chuo hicho  chenye mchepuo wa kilimo na stadi za mazingira ili kuchangia kuinua hali ya maisha ya watanzania haswa wanaoishi vijijini wakitegemea kilimo na ufugaji  kama uti wa mgongo wa maisha.

Aidha Daktari Katabaro alisema kuwa chuo kikuu cha Karagwe yaani Karagwe Universty  College(KARUCO) kitasaidia kuchochea matumizi ya zana za kisasa za uzalishaji na hivyo kuongeaza tija na kuboresha mazao mengi ya kilimo yanayozalishwa wilayani hapa.

Kwa upande wake  Askofu Daktari Benson   Bagonza  alisema kuwa chuo hicho  kitatoa fursa nyingi kwa wananchi zinazolenga  kutokomeza umaskini zikiwemo fursa ya elimu,Kiuchumi, kibiashara,kimiundo mbinu,kiafya na kimawasiliano.

Daktari Bagonza alisema kuwa licha ya kilimo na ufugaji  chuo kikuu kinakusudia  kuandaa walimu wenye  shahada  na stashahada  katika sanaa ,sayansi na biashara ili kuongeza idadi  ya walimu  hasa katika  shule za sekondari  wilayani  Karagwe.

Hata  hivyo Daktari  Bagonza alisema dayosisi itaendelea na jitihada za kushirikisha wadau mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi ili kupata fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho kuwa wapo wafadhili wa nje waliokwisha waunga mkono na kuonyesha dalili za kushirikiana na dayosisi katika mchakato huo.


Na
    Juhudi   Felix

KUSHUKA KWA ELIMU KATIKA MKOA WA KAGERA NA JUHUD FELIX

01: UTANGULIZI: Mkoa wa Kagera upo Magharibi mwa nchi yetu ya Tanzania. Unazo wilaya saba ambazo b Bukoba, Biharamulo, Chato, Karagwe, Missenyi, Muleba na Ngara. Makabila yaliyopo katika mkoa huu ni Wahaya, wanyambo, wahangaza, Wasubi na wasukuma. Mazao ya chakula ni ndizi, mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu, maharage na njugu mawe. Mazao ya biashara ni pamoja na
kahawa, pamba na ndizi. Mkoa wa Kagera hupata mvua katika msimu wa vuli na masika.

HALI YA ELIMU

Mkoa wa Kagera ulikuwa na hali nzuri sana ya kielimu kuanzia miaka ya 1960 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1980. Wananchi walikuwa na mwamko mkubwa sana wa elimu na vijana wengi walijiunga na shule za msingi wachache waliendelea na elimu ya sekondari katika shule za serikali na wachache  walikwenda kusoma katika shule za sekondari nchini Uganda. Elimu mkani Kagera ilipewa kipaumbele cha kwanza kwani wanafunzi waliokuwa na tatizo la upatikani wa mahitaji ya shule walipata msaada toka mfuko wa chama cha Ushirika na BCU(Buoba Cooperative Union) na hatimaye KCU 1990 LTDkupitia  mfuko wa Elimu (Balimi Education  Fund) Kutokana na jitihada za chama cha Ushirika cha Wakulima wa Kahawa (Buni) Kagera wanafunzi wengi waliendelea na masomo  yao hadi chuo kikuu. Wazazi na wananchi kwa ujumla walihakikisha watoto wote wenye uwezo wa kusoma wanasoma. Vijana waliohitimu Darasa la Nane, Kidato cha Nne na kuendelea masomo wengi walifanikiwa kupata ajira hivyo kuboresha maisha yao na familia zao. Mwanzoni mwa mwaka 1980 Elimu mkoani Kagera ilianza kuorora kutokana na sababu zifuatazo:-
1. VITA YA KAGERA:
Nchi yetu iliingia vitani na nchi ya Uganda maarufu kwa VITA YA KAGERA. Vita hivi vilisababisha watu wengi kupoteza maisha pamoja na mali zao. Ucchumi wa  mkoa na nchi yetu kwa ujumla ulidorora sana na maisha ya wananchi yalibadilika.
Vita ilidumu kwa muda mfupi lakini madhara yake yanaonekana hadi leo. Baada ya vita wanafunzi na watumishi wengi waliacha shule na kazi na kuingia kenye biashara na walitengeneza fedha nyingi kwa muda mfupi. Vijana wengi waliona nibora kufanyabiashara badala ya kuendelea na masomo shuleni. Wafanyakazi nao waliona ni bora kufanyabiasha kulikokuendelea na kazi za serikali ambazo zilikuwa hazilipi vizuri, kana kwamba hiyo haitoshi, ugonjwa wa UKIMWI ukaingia katika nchi yetu  ukitokea Uganda. Watu wengi walipoteza maisha bila kujua ni ugonjwa gani ulikuwa ukiwasumbua. Wanafamilia walitumia muda mwingi kuhudumia wagonjwa badala ya kufanya kazi  za uzalishaji mali ama wanafunzi kwenda shule. Pigo hilo linaendelea hadi leo. Pesa nyingi zilitumika kuboresha afya badala ya kulipia karo za wanafunzi.
Aidha  watoto wengi wanalazimika kujilea na kulea wadogo zao badala ya kuhudhuria shule.
2. KUSHUKA KWA BEI YA BUNI (KAHAWA)
Suala linalosababisha kudorora kwa elimu mkoani hapa ni kushuka vibaya kwa bei ya kahawa katika soko la dunia. Hali hii iliathiri sana uwezo wa wana Kagera kumudu gharama za masomo kwa watoto wao ndani na nje ya nchi. Aidha hali hii ilisababisha kuporomoka kwa chama cha KCU 1990 LTD pamoja na mfuko wa Elimu wa chama hicho uliojulikana kama “Balimi Education Fund”
3. UKOSEFU WA KAZI AU AJIRA:
Katikati ya miaka ya 1990 Serikali ilishindwa kuajiri watumishi wapya na mwishoni mwa miaka  hiyo ililazimika kupunguza watumishi wake (retrenchment) Watumishi waliopunguzwa katika sehemu zao za kazi walilipwa kiinua mgongo lakini fedha hizo ziliisha ndani ya muda mfupi na maisha yao yakawa katika hali mbaya. Vijana wengi walihangaika  huko na kule kutafuta ajira bila mafanikio na elimu yao ikaonekana haina maana yoyote.
4. MATARAJIO YA WAZAZI:
Wazazi walipokuwa wanatumia rasilimali zao kuwasomesha watoto wao walitazamia wapate kazi na wawasaidie kuwatunza wazazi wao pamoja na ndugu zao au familia zao. Baada ya wahitimu kukosa kazi wazazi walikata tamaa na kuvunjika moyo na hawakuona umuhimu wa kutumika rasilimali zao kuwasomesha watoto wakati hakuna ajira.
5. UGONJWA WA ZAO  LA MIGOMBA
Ugonjwa wa migomba maarufu kama “Myauko” umeongeza umasikini mkoani Kagera kwa sababu ni zao la chakula linalopendwa na watu wengi. Wananchi wananunua ndizi kwa bei kubwa na hivyo kukosa pesa za kuwalipia watoto wao gharama za kielimu.
      6. MWAMKO WA KIELIMU KATIKA MIKOA MINGINE
Tangu  enzi za uhueu wa nchi yetu mikoa iliyokuwa inaongoza kielimu ni Kilimanjaro, Mbeya na Kagera. Kwa sasa mikoa ambayo ilikuwa imejikita kwenye ufugaji na biashara za kuni na mkaa imeanza kukimbizana na elimu. Mkoa wetu upo pembezoni mwa nchi na hamna fursa kama mikoa ya wenzetu. Hali hii imeufanya mkoa wetu urudi nyuma zaidi kielimu maana ushindani umekua mkubwa zaidi.
7. JANGA LA MELI YA MV. BUKOBA
Kuzama kwa Meli ya Mv. Bukoba lilikuwa pigo kubwa kwa mkoa wetu maana walimu wengi waliopangwa Kagera waligoma kuja kwa kisingizio  ch kuogopa kuzama katika ziwa kwa vile njia ya uhakika wa kuja mkoani Kagera ilikuwa kupitia ziwa Viktoria mbaya zaidi hata vijana waliozaliwa Kagera baadhi yao waligoma kuja kufanya kazi hapo. Hali hii imesaidia sana kuishusha Kagera kielimu.
8. MATUMAINI MAPYA WANAKAGERA
Baada ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutuunganisha na mikoa jirani hali ya kielimu imeanza kuboreka Kagera. Mnamo miaka ya 1990 mkoa  Kagera ulikuwa unashika nafasi ya kumi na tisa kitaifa, lakini kwa sasa mkoa wa Kagera ni kati ya mikoa minne bora kielimu nchini.
9. JUKUMU LA MWANAKAGERA
Ni jukumu letu wana Kagera kuendeleza mkoa wetu kielimu. Elimu ni muhimu sana kwa watu wetu hata kama hakuna ajira ya kutosha. Hivyo kila mmoja kwa nafasi yake ajione kuwa anadeni la kuinua kiwango cha elimu. Ipo haja ya kuitisha mikutao ya hadhara ya kuhamasisha wananchi wafufue ari ya kuhakikisha watoto na wao wenyewe wanatoa kipaumbele cha kwanza kwa elimu. Walimu  wathaminiwe na wapewe ushirikiano wa kutosha kuitenda kazi yao.
Kamati za shule na WDC ziwashawishi wananchi  na wazazi kuchangia na kuindeleza elimu. Irudishwe mifumo ya wanakagera ya kuwasisia wazazi wa wanafunzi wenye kipato kidogo kwa mikopo yenye masharti nafuu , wale wote wanaopenda kijiendeleza kielimu. Watafutwe  wafadhili wa ndani na nje ya mkoa wa Kagera wawekeze katika Elimu hapa kwa gharama nafuu hasa kwa kujenga Vyuo Vikuu. Wanakagera waishio nje ya mkoa huu wawajibike kufufua umaarifa wa mkoa wao maana mkataa kwao hanatofauti na mtumwa.
Imeandaliwa na:

Idara ya Elimu ya Msingi
Manispaa ya Bukoba
21/01/2011
DARA YA UTUMISHI NA UTAWALA

UTANGULIZI

Idara ya utumishi na utawala  ni idara inayohusika moja kwa moja na usimamizi wa rasiliamli watu na kuhakikisha idara nyingine zinapangiwa watumishi kulingana  na Ikama  ya idara husika.

Halmashauri ya Manispaa  Bukoba ina jumla ya watumishi wapatao 1,205 kati  ya hao  watumishi 1148 wameajiriwa katika masharti ya kudumu na watumishi 57 ni watumishi wa muda (vibarua)

Idara ya utumishi ni idara mtambuka ambayo inahusika kupanga na kuandaa bajeti ya mishahara  ya watumishi  na kuhakikisha watumishi wanapata haki zao.

SHUGHULI ZINAZOFANYWA  NA IDARA

Baadhi ya majukumu yanayotekelezwa na idara hii ni pamoja na

i)             Kupandisha watumishi vyeo  kwa kushirikiana na bodi ya ajira na TSD Wilaya kwa upande wa walimu.

ii)           Kuthibitisha  watumishi kazini kwa kushirikiana na bodi ya ajira.

iii)          Kusimamia zoezi  zima la ujazaji wa fomu za OPRAS yaani upimaji wa kazi kwa watumishi

iv)          Kusimamia sheria, kanuni, zinazohusu watumishi

v)           Kushughulikia malipo kwa watumishi wanaostaafu kazi, mirathi na stahili nyingine.

vi)          Kuandaa mpango wa mafunzo kwa kupitia (TAA) Training Need  Assesment

Pamoja na kazi nyingine hizo ni baadhi ya kazi zinazofanywa na Idara hii.

CHANGAMOTO

i)             Bajeti  finyu ya mafunzo inayopelekea kutopatikana  fursa  ya kutosha  kwa watumishi  kwenda kwenye mafunzo

ii)           Upungufu wa watumishi hususan Idara ya Elimu, Afya  na kilimo.

iii)          Ukosefu wa vitendea kazi hususan kwa watendaji wa Kata na Mitaa.

iv)          Ukosefu na uelewa wa kanuni na sheria zinazohusu watumishi kwa  watumishi wenyewe.


Magedi Magezi,

Kaimu: Afisa Utumishi na Utawala

MANISPAA BUKOBA.
IDARA YA AFYA - KAGERA - BUKOBA
Kumb. Na. BMC/M.10/6/                                   26/1/2011

Mkurugenzi wa Manispaa
S. L. P. 284
BUKOBA

IDARA YA AFYA

Idara ya Afya, katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba inashughuli na utoaji wa huduma za tiba na kinga katika vituo 16 za kutolea huduma za Afya.


AINA YA KITUO
MMILIKI



Serikali
Mashirika ya Dini
Mashirika ya Umma
Binafsi
Jumla
1
Hospitali
1



1
2
Vituo vya Afya
2


1
3
3
Zahanati
8
1
1
2
12


Shughuli zinazofanyika

1.    Uagizaji na usambazaji wa madawa muhimu na vifaa vya kutolea huduma za afya
2.    Udhibiti wa magonjwa ya Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu na Ukoma
3.    Utoaji wa huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto.
4.    Utoaji wa huduma ya ukusanyaji na uzoaji wa taka ngumu (Udhibiti wa taka)
5.    Udhibiti wa magonjwa ya mlipuko na kukabiliana na majanga
6.    Ukaguzi wa majengo mbali mbali ya kuishi, biashara na taasisi na kuhimiza usafi
7.    Usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni za afya
8.    Utoaji wa elimu ya afya kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara, vikundi vya sanaa na vyombo vya habari.
9.    Ukaguzi wa maeneo ya wazi, makaburi, vyanzo vya maji, mifereji, viwanja vya michezo na maeneo ya mikusanyiko.


Mafanikio

1.    Kupungua kwa kiwango cha wagonjwa wa malaria kwa asilimia 2% kutoka 40.2% mwaka 2008 hadi 38.2% mwaka 2010.
2.    Kuongezeka kwa kiwango cha uchanjaji kutoka 89.1% mwaka 2009 hadi 90%.
3.    Kiwango cha maambukizi ya UKIMWI yamepungua kutoka 10.6% hadi 8.4% mwaka 2010 na jamii imehamasika kupata huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya UKIMWI
4.    Kuongezeka kwa vyombo vya kusomba taka ngumu kutoka magari/trekta 2 hadi 8 kwa msaada wa UN HABITAT (trekta 4 kubwa na 2 ndogo)
5.    Kujengwa kwa maghala (vizimba) 4 ya kuhihifadhia taka katika maeneo ya soko na yenye msongamano wa watu
6.    Halamashauri ilipokea magari 2 ya kubeba wagonjwa (Ambulance) na kupeleka Kituo cha Afya Rwamishenye na Zahanati ya Kashai

Changamoto

1.    Upungufu wa madawa muhimu kulingana na mahitaji ya vituo
2.    Ukosefu wa matanuru ya kuchoma taka zilizosibika (taka za hospitali)
3.    Ufinyu wa bajeti ya kwa ajili ya utoaji wa huduma za afya ikiwemo usafi
4.    Utiririshaji ovyo wa maji taka mitaani na kwenye mifereji ya maji ya mvua na hatimaye kwenye vyanzo vya maji.
5.    Kujaa kwa eneo la makaburi ya Kishenge na kutokuwepo kwa eneo mbadala kwa ajili ya maziko
6.    Ukosefu wa maeneo ya kukusanyia taka katika maeneo mbali mbali ya Kata hasa kata za mjini kati
7.    Sekta binafsi na asasi za kijamii kutofanya kufanya shughuli za usafi katika eneo la Manispaa kama wakala.
8.    Upungufu wa watumishi wa kada mbali mbali
9.    Ujenzi holela wa makazi katika maeneo oevu, kando kando ya vyanzo vya maji (mto Kanoni) na kwenye maeneo yenye mawe.
10. Uchakavu wa miundo mbinu hasa mifereji ya maji ya mvua katika maeneo ya barabara za Manispaa
11. Kutobomolewa kwa baadhi ya vichochoro katika maeneo kadhaa za Manispaa
12. Kuzagaa kwa wafanya biashara ndogo ndogo (wamachinga) katika mitaa mbali mbali eneo la mjini kati ambao ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira ya mji.
13. Wananchi kutozingatia sheria na kanuni za kiafya.
14. Ukosefu wa miundo mbinu thabiti (pavement) katika barabara zote za lami na kusababisha mchanga kujaa barabarani hatimaye kujaa na kuziba mitaro.
15. Upungufu wa vyoo vya umma katika maeneo mengi yenye shughuli za kijamii na biashara
16. Ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, mifereji, maji nk katika maeneo yenye msongamano (squatters)

Mikakati/Mwelekeo:-

1.    Kuomba madawa kutoka Bohari Kuu ya madawa (MSD) kulingana na mahitaji ya vituo vyetu na kuweka bajeti ya nyongeza mwaka 2011/2012
2.    Kuendelea kuhamasisha jamii kuwa na tabia ya kujitokeza kupima afya zao kwa hiari na kupata ushauri nasaha
3.    Kuweka bajeti kwa ajili ya ujenzi wa matanuru ya kuchomea taka za hospitali
4.    Kuhimiza Halmashauri kutenga eneo jipya la makaburi na kuliwekea uzio tayari kwa matumizi sanjari na kufunga eneo liliojaa la makaburi ya Kishenge
5.    Kuhimiza Kamati za Maendeleo za Kata na Mitaa kutenga maeneo ya kukusanyia taka kabla ya kupelekwa dampo
6.    Kuomba kibali cha kuajiri watumishi wa kada mbali mbali hasa madereva kwa magari ya taka.
7.    Kuhamasisha asasi za kijamii na binafsi kufanya shughuli za usafi wa Manispaa.
8.    Kudhibiti ujenzi holela katika maeneo ya vyanzo vya maji hasa mto Kanoni na maeneo oevu kwa kushirikisha Idara ya Mipango Miji na Uhandisi
9.    Kukarabati mifereji mibovu ya maji ya mvua katika maeneo mbalimbali ya barabara za Manispaa kulingana na bajeti
10. Kupitia mikakati iliyopo ya usafi wa mazingira kwa kutambua ufanisi/upungufu na kuboresha kulingana na rasilimali zilizopo.
11. Kuwafikisha mahakamani watu wote ambao wanakiuka sheria na kanuni za afya katika mahakama ya papo kwa papo.
12. Kuendelea kuhamasisha jamii kubadili mtazamo na tabia ya kuzingatia usafi na kuchukia uchafu kusudi kuboresha afya na usafi wa mazingira
13. Kuendelea na mikakati ya ukaguzi wa majengo ya kuishi, taasisi na biashara na kuhimiza usafi.
14. Kuhamasisha na kuhimiza wananchi kushiriki kuweka safi maeneo yao kila wiki, siku ya alhamisi ambayo ni Siku ya Usafi katika Manispaa.
15. Usafi wa Manispaa kuwa miongoni mwa vipaumbele katika mipango ya Halmashauri kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2011/2012.
16. Kushirikisha sekta binafsi na asasi za kijamii kujenga vyoo vya umma katika maeneo mbali mbali yenye mikusanyiko ya watu.


Dr. Raphael Kiula
MGANGA MKUU WA MANISPAA
BUKOBA
UFANISI NA CHANGAMOTO ZA SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII

HALI YA UTENDAJI KAZI
Watendaji wapo wanne, miongononi mwao mmoja ni mkuu wa idara na mwingine ni mratibu wa TASAF. SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA IDARA
UTOAJI WA MIKOPO
Jumla ya vikundi 12 vya wanawake na kimoja cha vijana vimepata mkopo kwa
kipindi cha mwaka 2009 hadi 2011.
 CHANGAMOTO
Baadhi ya vikundi havirejeshi mkopo kwa wakati hivyo kusababisha udumavu wa mfuko wa wanawake na vijana.
HUDUMA NA MISAADA
 Kulipa karo na mahitaji muhimu kwa wanafunzi yatima walioko SekondariØ na vyuo mbalimbali. Kwa kipindi cha mwaka 2010 zaidi ya sh. 11,000,000/= zimetumika katika shuguli hii. Vikundi vingine 19 vilipata mkopo usiyo na riba kupitia mfuko wa microkrediti tangu mwaka 2009 hadi 2010.
 Wanawake 50 waishio na VVU/UKIMWI wamepewa msaada wa lishe.Ø
CHANGAMOTO
 Idadi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumuØ wanaohitaji msaada wa masomo  ni kubwa sana ukilinganisha na fedha ambazo kwa kiasi kikubwa zinazotolewa na wahisani kwa ajili ya kuwalipia gharama za masomo hivyo kutofikia malengo yaliyopangwa.
 Baadhi ya vikundi vilivyokopa kupita mfuko wa microcredit mwaka 2009Ø havijarejesha na hivyo kufanya kiasi cha deni kuwa shilingi 2,545,272.45/=
KUTOA ELIMU
Mafunzo ya ujasiliamali
Vikundi mbalimbali vya ujasiliamali vimekuwa vikipata elimu hususani kabla ya kuanzisha vikundi. Jumla ya Wanawake 55 waishio na UVV/UKIMWI wamepewa mafunzo ya ujasiliamali na kuhamasisha  waanzishe vikundi kwa ajili ya kupatiwa mikopo, mafunzo haya yalitolewa mwaka 2010.
CHANGAMOTO
 Baadhi ya vikundi vinahitaji zaidi ruzuku kuliko mikopo kwa sababu yaØ kutokujiamini katika shughuli zao hivyo wanahofia hasara ambayo inaweza kusababisha kushindwa kurejesha kwa wakati.
Elimu ya UKIMWI
Elimu ya UKIMWI imekuwa ikitolewa katika jamii kwa mfano kipindi cha mwaka 2010 elimu hii imetolewa kwa Watumishi 40 wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba  namna ya kujikinga na VVU, kuepuka maambukizi mapya na maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
CHANGAMOTO
Unyanyapaa bado ni tatizo katika utekelezaji wa shughuli za UKIMWI kwa sababu waathirika wengi bado hawajajiweka wazi na hili linaweza kuchochea maambukizi mapya.

Mchango wa KKKT Dayosisi ya Karagwe katika maendeleo ya jamii.

Askofu wa Dayosisi ya Karagwe Mh.  Dr. Benson Bagonza akiwa na wageni walioitembelea dayosisi toka Sweden mapema mwaka 2011 (Picha na Mchg.Oscar Samwel).
Dayosisi ya Karagwe ni miongoni mwa dayosisi ishirini zinazounda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Dayosisi ya Karagwe ilizinduliwa
rasmi tarehe 7/1/1979 pale Lukajange.

Tangu wakati huo dayosisi ya Karagwe imeendelea kujihusisha na maisha ya jamii ya wana Karagwe kwa kutoa huduma za kijamii na kuendesha shughuli za maendeleo katika wilaya za Karagwe na Ngara. Huduma zote zinazotolewa na Dayosisi ya Karagwe huwalenga wanajamii wote bila kujali dini zao, kabila wala rangi zao.
Zifuatazo ni huduma za maendeleo ambazo hutolewa na Dayosisi ya Karagwe.
1. Huduma za Afya- Dayosisi ya Karagwe inamiliki Hospitali ya Nyakahanga ambayo ndiyo hospitali teule ya wilaya ya Karagwe.Hospitali hii ni mkombozi kwa jamii ya watu wa Karagwe na maeneo jirani kama wilaya mpya ya Misenye. Huduma za kinga na tiba hutolewa katika hospitali hii.Pia hutoa huduma nyingine kama huduma ya afya ya msingi, upimaji wa virusi vya Ukimwi kwa hiari (ANGAZA), kliniki kwa ajili ya akina mama waja wazito nk. Pia hospitali ya Nyakahanga inaendesha na kusimamia zahanati nyingine nne ambazo ni Nyakatera, Ibamba-Mabira, zahanati ya shule ya sekondari Karagwe na Katenga-Ngara.
2. Mradi wa kudhibiti Ukimwi- Kutokana na janga la ugonjwa wa Ukimwi unaowatesa watu wengi, dayosisi ya Karagwe iliamua kuanzisha mradi huu ili kuwasaidia watu katika jamii ya Karagwe kwa kuwapatia elimu juu Ukimwi, kusaidia yatima hasa kuwalipia karo na mahitaji mengine kwa kusaidiana na familia, kutoa chakula kwa wanaoishi na VVU pamoja na mambo ya haki na utetezi hasa kwa wajane ambao kwa njia moja au nyingine huwa katika hatari ya kukosa haki zao katika familia za waume zao.


        Kilimo cha umwagiliaji Ihembe (Picha na Mchg.Oscar Samwel
3. Udiakonia na utetezi-Dayosisi ya Karagwe inawajibika katika kufanya shughuli za diakonia ikiwa ni kuwasaidia wasijiweza au watu ambao wanaishi katika mazingira hatarishi. Hapa makundi ya watu kama wazee, walemavu, wenye mtindio wa akili, nk husaidiwa katika kupatiwa mahitaji ya lazima ikiwemo chakula, mavazi, kuwajengea nyumba, kuwanunulia mashamba na kuwatetea wale walio katika hatari ya kukosa haki zao.Vilevile kitengo cha diakonia hutoa msaada wa mbuzi watano kwa kila familia iliyobainishwa kuwa maskini ili kwa njia hiyo mradi huo wa mbuzi uwasaidie kuongeza kipato cha familia ili waweze kujipatia mahitaji ya msingi pale nyumbani.  Pia kitengo hiki cha diakonia hutoa elimu kwa jamii ili ione umuhimu na wajibu katika kuwasaidia wenye shida maana wanaishi nao katia jamii moja.
4. Elimu- Hii pia ni sehemu muhimu ya kazi ya dayosisi ya Karagwe. Mpaka sasa dayosisi ya Karagwe inamiliki shule mbili za Sekondari ambazo ni Shule ya Sekondari Karagwe (KARASECO) na Shule ya Sekondari ya wasichana Bweranyamge. Katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2010 KARASECO imeshika nafasi ya pili (2) kimkoa kati ya shule 155 zenye idadi ya wanafunzi zaidi ya arobaini na ya 44 kitaifa kati ya shule 3196. Bweranyange imeshika nafasi 4 kimkoa kati ya shule 32 zenye wanafunzi chini ya 40 na ya 64 kitaifa kati ya shule 490. Pia dayosisi inamiliki shule mbili za kiingereza ambazo ni Tegemeo (English Medium) na Imani (English Medium). Vituo vingine vya elimu ni kama ifuatavyo: Chuo cha Biblia Nkwenda, Chuo cha ufundi na kilimo Nkwenda, Chuo cha ufundi staid kwa watoto yatima Lukajange, Chuo cha udiakonia na waalimu wa shule za awali Nkwenda. Pia katika upande wa elimu,dayosisi ya Karagwe inao mpango maalumu wa kuanzisha chuo kikuu hapa Karagwe na mipango inaendelea vizuri kwa matumaini kwamba chuo hiki kitaweza kuanza kupokea wanafunzi mwaka 2013 kama mipango yote itaenda kama ilivyopangwa.Ikumbukwe kwamba huduma zote za elimu hutolewa kwa watu wote bila kujali dini wala kabila.
5. Miradi ya Maendeleo: Dayosisi pia inasimamia miradi ya maendeleo kwa ajili ya jamii ya Karagwe na watu wengine wote kama ifuatavyo:Karagwe Hotel and guest house: Hiki ni kituo ambacho hutoa huduma za malazi chakula na ukumbi wa mikutano. Watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi hufurahia kutumia kituo hiki kwa sababu ya huduma zake bora, uaminifu wa wahudumu na utulivu uliop sehemu hiyo. Unafuu wa bei pia huwavutia watumiaji maana bei zetu zinalenga huduma zaidi kuliko biashara.  Miradi mingine ni kama mashine za kusaga nafaka huko majimboni, miradi ya maji, upandaji miti, uwanja wa Ndege Ihanda, miradi ya wanawake ya kuinua kipato chao kama ufugaji wa kuku, ushonaji nk

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana BweranyangeDayosisi ya Karagwe (Picha na Mchg.Oscar Samwel
6. Mradi wa utunzaji wa mazingira: Dayosisi ya Karagwe iko mstari wa mbele katika kutunza mazingira kwa kuamini kwamba mazingira ni uhai. Mradi huu unahusisha majimbo yote, sharika na mitaa ambapo inasisitizwa kwamba maeneo yote ya Kanisa yapandwe miti. Kwa mfano: Mwaka 2011 katika majimbo ya Mabira, Murongo, Bweranyange na Kyerwa jumla ya miti 500.000 ilipandwa chini ya mradi huu ambao uliazishwa mwaka 2004. Katika harakati hizi za utunzaji mazingira, dayosisi ya Karagwe kwa kushirikiana na Jimbo rafiki huko Ujerumani imeanzisha mradi wa mazingira uitwao KAKAUMAKI (Kampeni Kabambe ya Utunzaji mazingira Kituntu). Mradi huu unatekelezwa katika Jimbo la Kituntu na kwa mwaka jana jumla ya miti 17,500 ilipandwa. Pia dayosisi ya Karagwe inahimiza vituo vyake vyote ikiwemo mashule na vituo vingine kuhakikisha wanapanda miti kwa wingi ambayo mbali na kutunza mazingira lakini pia huko mbele ya safari itakuwa kitegauchumi pindi itakapovunwa.
7. Mradi wa Maisha mapya (New life in Karagwe) Huu ni mradi ambao ulianzishwa mwaka 2006 na unalenga kuwawezesha wanajamii kubadili maisha yao toka hali duni ya kipato hadi kupata hali nzuri na kumudu kutunza familia zao. Mradi huu unahusika na kuwasaidia wakulima waweze kulima kwa kutumia mbinu za kisasa ambapo mkulima hupewa Ng’ombe mmoja jike ili pamoja na kupata maziwa lakini pia mkulima hupata mbolea kwa ajili ya shamba lake na hivyo kipato cha familia kuongezeka. Upande wa wanawake wajane wao hupewa mbuzi wa maziwa. Mpaka sasa jumla ya Ng’ombe 300 na mbuzi 100 tayari wamegawiwa kwa walengwa. Pia semina hutolewa kwa wakulima jinsi ya kulima kwa tija na kutunza mazingira. Wakulima hupata nafasi ya kutembelea maeneo ya kilimo ili kujifunza kwa vitendo.Mfano mwaka 2010 wakulima walitembelea Maruku Bukoba na Igabiro ambapo walipata nafasi ya kujifunza kwa vitendo. Kadhalika mradi huu unawaelimisha watu juu ya utunzaji mazingira


8. Mradi wa kujengea uwezo watoto wa kike (wasichana): Mradi huu ni kwa ajili ya kuwasaidia wasichana walio katika umri mdogo vijijini na hata mashuleni ili waweze kujitambua na kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, ubakaji nk. Pia hufundishwa na kuelekezwa juu ya haki zao za msingi ili waweze kujitetea mbele ya jamii. Mbali na hayo pia mradi huu unalenga kuwabaini wasichana ambao kwa sababu za umaskini wa familia zao wameshindwa kuingia sekondari kwa kukosa karo. Wakishabainiwa mradi unawasaidia kuwalipia karo na mahitaji ya shule, mpango huu utaanza rasmi mwaka huu.
9. SACCOS: Huu ni mpango wa kuwasaidia wananchi ili waweze kuweka na kukopa kupitia vikundi vyao vya SACCOS ambao ulianza rasmi mwaka 2009. Mpaka sasa jumla ya Saccos 8 tayari zimesajiliwa katika majimbo ya Ihembe na Bweranyange. Kitengo cha Saccos ambaocho kiko makao makuu ya dayosisi Lukajange huwasaidia wanachama kuwapatia elimu kwa njia ya semina, kuwapa vitendea kazi hasa wakati wa kuanza kama vitabu, kasiki, nk. Pia kwa sasa wako katika kuziwezesha Saccos hizo kujenga ofisi za kuduma ambapo kikundi husaidiwa kupewa mabati, sementi, milango na madirisha ya chuma,vifaa vingine ni mchango wa wanachama.

Imeandaliwa na Mchg. Oscar S. Samwel





Baadhi ya habari zilizoko kwenye maktaba yangu ambazo ninataka niwajulishe au kuwarejesha kidogo ktk Karagwe yetu tunayoipenda tegemea nyingine zilizo current haswa upande wa elimu ambao tuko nyuma hatu kidato cha tano na sita kwa shule za serikali hii ni hatari nitawajuza tutakuwa na mjadala wa pamoja.