Thursday, 3 November 2011

KUSHUKA KWA ELIMU KATIKA MKOA WA KAGERA NA JUHUD FELIX

01: UTANGULIZI: Mkoa wa Kagera upo Magharibi mwa nchi yetu ya Tanzania. Unazo wilaya saba ambazo b Bukoba, Biharamulo, Chato, Karagwe, Missenyi, Muleba na Ngara. Makabila yaliyopo katika mkoa huu ni Wahaya, wanyambo, wahangaza, Wasubi na wasukuma. Mazao ya chakula ni ndizi, mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu, maharage na njugu mawe. Mazao ya biashara ni pamoja na
kahawa, pamba na ndizi. Mkoa wa Kagera hupata mvua katika msimu wa vuli na masika.

HALI YA ELIMU

Mkoa wa Kagera ulikuwa na hali nzuri sana ya kielimu kuanzia miaka ya 1960 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1980. Wananchi walikuwa na mwamko mkubwa sana wa elimu na vijana wengi walijiunga na shule za msingi wachache waliendelea na elimu ya sekondari katika shule za serikali na wachache  walikwenda kusoma katika shule za sekondari nchini Uganda. Elimu mkani Kagera ilipewa kipaumbele cha kwanza kwani wanafunzi waliokuwa na tatizo la upatikani wa mahitaji ya shule walipata msaada toka mfuko wa chama cha Ushirika na BCU(Buoba Cooperative Union) na hatimaye KCU 1990 LTDkupitia  mfuko wa Elimu (Balimi Education  Fund) Kutokana na jitihada za chama cha Ushirika cha Wakulima wa Kahawa (Buni) Kagera wanafunzi wengi waliendelea na masomo  yao hadi chuo kikuu. Wazazi na wananchi kwa ujumla walihakikisha watoto wote wenye uwezo wa kusoma wanasoma. Vijana waliohitimu Darasa la Nane, Kidato cha Nne na kuendelea masomo wengi walifanikiwa kupata ajira hivyo kuboresha maisha yao na familia zao. Mwanzoni mwa mwaka 1980 Elimu mkoani Kagera ilianza kuorora kutokana na sababu zifuatazo:-
1. VITA YA KAGERA:
Nchi yetu iliingia vitani na nchi ya Uganda maarufu kwa VITA YA KAGERA. Vita hivi vilisababisha watu wengi kupoteza maisha pamoja na mali zao. Ucchumi wa  mkoa na nchi yetu kwa ujumla ulidorora sana na maisha ya wananchi yalibadilika.
Vita ilidumu kwa muda mfupi lakini madhara yake yanaonekana hadi leo. Baada ya vita wanafunzi na watumishi wengi waliacha shule na kazi na kuingia kenye biashara na walitengeneza fedha nyingi kwa muda mfupi. Vijana wengi waliona nibora kufanyabiashara badala ya kuendelea na masomo shuleni. Wafanyakazi nao waliona ni bora kufanyabiasha kulikokuendelea na kazi za serikali ambazo zilikuwa hazilipi vizuri, kana kwamba hiyo haitoshi, ugonjwa wa UKIMWI ukaingia katika nchi yetu  ukitokea Uganda. Watu wengi walipoteza maisha bila kujua ni ugonjwa gani ulikuwa ukiwasumbua. Wanafamilia walitumia muda mwingi kuhudumia wagonjwa badala ya kufanya kazi  za uzalishaji mali ama wanafunzi kwenda shule. Pigo hilo linaendelea hadi leo. Pesa nyingi zilitumika kuboresha afya badala ya kulipia karo za wanafunzi.
Aidha  watoto wengi wanalazimika kujilea na kulea wadogo zao badala ya kuhudhuria shule.
2. KUSHUKA KWA BEI YA BUNI (KAHAWA)
Suala linalosababisha kudorora kwa elimu mkoani hapa ni kushuka vibaya kwa bei ya kahawa katika soko la dunia. Hali hii iliathiri sana uwezo wa wana Kagera kumudu gharama za masomo kwa watoto wao ndani na nje ya nchi. Aidha hali hii ilisababisha kuporomoka kwa chama cha KCU 1990 LTD pamoja na mfuko wa Elimu wa chama hicho uliojulikana kama “Balimi Education Fund”
3. UKOSEFU WA KAZI AU AJIRA:
Katikati ya miaka ya 1990 Serikali ilishindwa kuajiri watumishi wapya na mwishoni mwa miaka  hiyo ililazimika kupunguza watumishi wake (retrenchment) Watumishi waliopunguzwa katika sehemu zao za kazi walilipwa kiinua mgongo lakini fedha hizo ziliisha ndani ya muda mfupi na maisha yao yakawa katika hali mbaya. Vijana wengi walihangaika  huko na kule kutafuta ajira bila mafanikio na elimu yao ikaonekana haina maana yoyote.
4. MATARAJIO YA WAZAZI:
Wazazi walipokuwa wanatumia rasilimali zao kuwasomesha watoto wao walitazamia wapate kazi na wawasaidie kuwatunza wazazi wao pamoja na ndugu zao au familia zao. Baada ya wahitimu kukosa kazi wazazi walikata tamaa na kuvunjika moyo na hawakuona umuhimu wa kutumika rasilimali zao kuwasomesha watoto wakati hakuna ajira.
5. UGONJWA WA ZAO  LA MIGOMBA
Ugonjwa wa migomba maarufu kama “Myauko” umeongeza umasikini mkoani Kagera kwa sababu ni zao la chakula linalopendwa na watu wengi. Wananchi wananunua ndizi kwa bei kubwa na hivyo kukosa pesa za kuwalipia watoto wao gharama za kielimu.
      6. MWAMKO WA KIELIMU KATIKA MIKOA MINGINE
Tangu  enzi za uhueu wa nchi yetu mikoa iliyokuwa inaongoza kielimu ni Kilimanjaro, Mbeya na Kagera. Kwa sasa mikoa ambayo ilikuwa imejikita kwenye ufugaji na biashara za kuni na mkaa imeanza kukimbizana na elimu. Mkoa wetu upo pembezoni mwa nchi na hamna fursa kama mikoa ya wenzetu. Hali hii imeufanya mkoa wetu urudi nyuma zaidi kielimu maana ushindani umekua mkubwa zaidi.
7. JANGA LA MELI YA MV. BUKOBA
Kuzama kwa Meli ya Mv. Bukoba lilikuwa pigo kubwa kwa mkoa wetu maana walimu wengi waliopangwa Kagera waligoma kuja kwa kisingizio  ch kuogopa kuzama katika ziwa kwa vile njia ya uhakika wa kuja mkoani Kagera ilikuwa kupitia ziwa Viktoria mbaya zaidi hata vijana waliozaliwa Kagera baadhi yao waligoma kuja kufanya kazi hapo. Hali hii imesaidia sana kuishusha Kagera kielimu.
8. MATUMAINI MAPYA WANAKAGERA
Baada ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutuunganisha na mikoa jirani hali ya kielimu imeanza kuboreka Kagera. Mnamo miaka ya 1990 mkoa  Kagera ulikuwa unashika nafasi ya kumi na tisa kitaifa, lakini kwa sasa mkoa wa Kagera ni kati ya mikoa minne bora kielimu nchini.
9. JUKUMU LA MWANAKAGERA
Ni jukumu letu wana Kagera kuendeleza mkoa wetu kielimu. Elimu ni muhimu sana kwa watu wetu hata kama hakuna ajira ya kutosha. Hivyo kila mmoja kwa nafasi yake ajione kuwa anadeni la kuinua kiwango cha elimu. Ipo haja ya kuitisha mikutao ya hadhara ya kuhamasisha wananchi wafufue ari ya kuhakikisha watoto na wao wenyewe wanatoa kipaumbele cha kwanza kwa elimu. Walimu  wathaminiwe na wapewe ushirikiano wa kutosha kuitenda kazi yao.
Kamati za shule na WDC ziwashawishi wananchi  na wazazi kuchangia na kuindeleza elimu. Irudishwe mifumo ya wanakagera ya kuwasisia wazazi wa wanafunzi wenye kipato kidogo kwa mikopo yenye masharti nafuu , wale wote wanaopenda kijiendeleza kielimu. Watafutwe  wafadhili wa ndani na nje ya mkoa wa Kagera wawekeze katika Elimu hapa kwa gharama nafuu hasa kwa kujenga Vyuo Vikuu. Wanakagera waishio nje ya mkoa huu wawajibike kufufua umaarifa wa mkoa wao maana mkataa kwao hanatofauti na mtumwa.
Imeandaliwa na:

Idara ya Elimu ya Msingi
Manispaa ya Bukoba
21/01/2011
DARA YA UTUMISHI NA UTAWALA

UTANGULIZI

Idara ya utumishi na utawala  ni idara inayohusika moja kwa moja na usimamizi wa rasiliamli watu na kuhakikisha idara nyingine zinapangiwa watumishi kulingana  na Ikama  ya idara husika.

Halmashauri ya Manispaa  Bukoba ina jumla ya watumishi wapatao 1,205 kati  ya hao  watumishi 1148 wameajiriwa katika masharti ya kudumu na watumishi 57 ni watumishi wa muda (vibarua)

Idara ya utumishi ni idara mtambuka ambayo inahusika kupanga na kuandaa bajeti ya mishahara  ya watumishi  na kuhakikisha watumishi wanapata haki zao.

SHUGHULI ZINAZOFANYWA  NA IDARA

Baadhi ya majukumu yanayotekelezwa na idara hii ni pamoja na

i)             Kupandisha watumishi vyeo  kwa kushirikiana na bodi ya ajira na TSD Wilaya kwa upande wa walimu.

ii)           Kuthibitisha  watumishi kazini kwa kushirikiana na bodi ya ajira.

iii)          Kusimamia zoezi  zima la ujazaji wa fomu za OPRAS yaani upimaji wa kazi kwa watumishi

iv)          Kusimamia sheria, kanuni, zinazohusu watumishi

v)           Kushughulikia malipo kwa watumishi wanaostaafu kazi, mirathi na stahili nyingine.

vi)          Kuandaa mpango wa mafunzo kwa kupitia (TAA) Training Need  Assesment

Pamoja na kazi nyingine hizo ni baadhi ya kazi zinazofanywa na Idara hii.

CHANGAMOTO

i)             Bajeti  finyu ya mafunzo inayopelekea kutopatikana  fursa  ya kutosha  kwa watumishi  kwenda kwenye mafunzo

ii)           Upungufu wa watumishi hususan Idara ya Elimu, Afya  na kilimo.

iii)          Ukosefu wa vitendea kazi hususan kwa watendaji wa Kata na Mitaa.

iv)          Ukosefu na uelewa wa kanuni na sheria zinazohusu watumishi kwa  watumishi wenyewe.


Magedi Magezi,

Kaimu: Afisa Utumishi na Utawala

MANISPAA BUKOBA.
IDARA YA AFYA - KAGERA - BUKOBA
Kumb. Na. BMC/M.10/6/                                   26/1/2011

Mkurugenzi wa Manispaa
S. L. P. 284
BUKOBA

IDARA YA AFYA

Idara ya Afya, katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba inashughuli na utoaji wa huduma za tiba na kinga katika vituo 16 za kutolea huduma za Afya.


AINA YA KITUO
MMILIKI



Serikali
Mashirika ya Dini
Mashirika ya Umma
Binafsi
Jumla
1
Hospitali
1



1
2
Vituo vya Afya
2


1
3
3
Zahanati
8
1
1
2
12


Shughuli zinazofanyika

1.    Uagizaji na usambazaji wa madawa muhimu na vifaa vya kutolea huduma za afya
2.    Udhibiti wa magonjwa ya Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu na Ukoma
3.    Utoaji wa huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto.
4.    Utoaji wa huduma ya ukusanyaji na uzoaji wa taka ngumu (Udhibiti wa taka)
5.    Udhibiti wa magonjwa ya mlipuko na kukabiliana na majanga
6.    Ukaguzi wa majengo mbali mbali ya kuishi, biashara na taasisi na kuhimiza usafi
7.    Usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni za afya
8.    Utoaji wa elimu ya afya kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara, vikundi vya sanaa na vyombo vya habari.
9.    Ukaguzi wa maeneo ya wazi, makaburi, vyanzo vya maji, mifereji, viwanja vya michezo na maeneo ya mikusanyiko.


Mafanikio

1.    Kupungua kwa kiwango cha wagonjwa wa malaria kwa asilimia 2% kutoka 40.2% mwaka 2008 hadi 38.2% mwaka 2010.
2.    Kuongezeka kwa kiwango cha uchanjaji kutoka 89.1% mwaka 2009 hadi 90%.
3.    Kiwango cha maambukizi ya UKIMWI yamepungua kutoka 10.6% hadi 8.4% mwaka 2010 na jamii imehamasika kupata huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya UKIMWI
4.    Kuongezeka kwa vyombo vya kusomba taka ngumu kutoka magari/trekta 2 hadi 8 kwa msaada wa UN HABITAT (trekta 4 kubwa na 2 ndogo)
5.    Kujengwa kwa maghala (vizimba) 4 ya kuhihifadhia taka katika maeneo ya soko na yenye msongamano wa watu
6.    Halamashauri ilipokea magari 2 ya kubeba wagonjwa (Ambulance) na kupeleka Kituo cha Afya Rwamishenye na Zahanati ya Kashai

Changamoto

1.    Upungufu wa madawa muhimu kulingana na mahitaji ya vituo
2.    Ukosefu wa matanuru ya kuchoma taka zilizosibika (taka za hospitali)
3.    Ufinyu wa bajeti ya kwa ajili ya utoaji wa huduma za afya ikiwemo usafi
4.    Utiririshaji ovyo wa maji taka mitaani na kwenye mifereji ya maji ya mvua na hatimaye kwenye vyanzo vya maji.
5.    Kujaa kwa eneo la makaburi ya Kishenge na kutokuwepo kwa eneo mbadala kwa ajili ya maziko
6.    Ukosefu wa maeneo ya kukusanyia taka katika maeneo mbali mbali ya Kata hasa kata za mjini kati
7.    Sekta binafsi na asasi za kijamii kutofanya kufanya shughuli za usafi katika eneo la Manispaa kama wakala.
8.    Upungufu wa watumishi wa kada mbali mbali
9.    Ujenzi holela wa makazi katika maeneo oevu, kando kando ya vyanzo vya maji (mto Kanoni) na kwenye maeneo yenye mawe.
10. Uchakavu wa miundo mbinu hasa mifereji ya maji ya mvua katika maeneo ya barabara za Manispaa
11. Kutobomolewa kwa baadhi ya vichochoro katika maeneo kadhaa za Manispaa
12. Kuzagaa kwa wafanya biashara ndogo ndogo (wamachinga) katika mitaa mbali mbali eneo la mjini kati ambao ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira ya mji.
13. Wananchi kutozingatia sheria na kanuni za kiafya.
14. Ukosefu wa miundo mbinu thabiti (pavement) katika barabara zote za lami na kusababisha mchanga kujaa barabarani hatimaye kujaa na kuziba mitaro.
15. Upungufu wa vyoo vya umma katika maeneo mengi yenye shughuli za kijamii na biashara
16. Ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, mifereji, maji nk katika maeneo yenye msongamano (squatters)

Mikakati/Mwelekeo:-

1.    Kuomba madawa kutoka Bohari Kuu ya madawa (MSD) kulingana na mahitaji ya vituo vyetu na kuweka bajeti ya nyongeza mwaka 2011/2012
2.    Kuendelea kuhamasisha jamii kuwa na tabia ya kujitokeza kupima afya zao kwa hiari na kupata ushauri nasaha
3.    Kuweka bajeti kwa ajili ya ujenzi wa matanuru ya kuchomea taka za hospitali
4.    Kuhimiza Halmashauri kutenga eneo jipya la makaburi na kuliwekea uzio tayari kwa matumizi sanjari na kufunga eneo liliojaa la makaburi ya Kishenge
5.    Kuhimiza Kamati za Maendeleo za Kata na Mitaa kutenga maeneo ya kukusanyia taka kabla ya kupelekwa dampo
6.    Kuomba kibali cha kuajiri watumishi wa kada mbali mbali hasa madereva kwa magari ya taka.
7.    Kuhamasisha asasi za kijamii na binafsi kufanya shughuli za usafi wa Manispaa.
8.    Kudhibiti ujenzi holela katika maeneo ya vyanzo vya maji hasa mto Kanoni na maeneo oevu kwa kushirikisha Idara ya Mipango Miji na Uhandisi
9.    Kukarabati mifereji mibovu ya maji ya mvua katika maeneo mbalimbali ya barabara za Manispaa kulingana na bajeti
10. Kupitia mikakati iliyopo ya usafi wa mazingira kwa kutambua ufanisi/upungufu na kuboresha kulingana na rasilimali zilizopo.
11. Kuwafikisha mahakamani watu wote ambao wanakiuka sheria na kanuni za afya katika mahakama ya papo kwa papo.
12. Kuendelea kuhamasisha jamii kubadili mtazamo na tabia ya kuzingatia usafi na kuchukia uchafu kusudi kuboresha afya na usafi wa mazingira
13. Kuendelea na mikakati ya ukaguzi wa majengo ya kuishi, taasisi na biashara na kuhimiza usafi.
14. Kuhamasisha na kuhimiza wananchi kushiriki kuweka safi maeneo yao kila wiki, siku ya alhamisi ambayo ni Siku ya Usafi katika Manispaa.
15. Usafi wa Manispaa kuwa miongoni mwa vipaumbele katika mipango ya Halmashauri kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2011/2012.
16. Kushirikisha sekta binafsi na asasi za kijamii kujenga vyoo vya umma katika maeneo mbali mbali yenye mikusanyiko ya watu.


Dr. Raphael Kiula
MGANGA MKUU WA MANISPAA
BUKOBA
UFANISI NA CHANGAMOTO ZA SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII

HALI YA UTENDAJI KAZI
Watendaji wapo wanne, miongononi mwao mmoja ni mkuu wa idara na mwingine ni mratibu wa TASAF. SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA IDARA
UTOAJI WA MIKOPO
Jumla ya vikundi 12 vya wanawake na kimoja cha vijana vimepata mkopo kwa
kipindi cha mwaka 2009 hadi 2011.
 CHANGAMOTO
Baadhi ya vikundi havirejeshi mkopo kwa wakati hivyo kusababisha udumavu wa mfuko wa wanawake na vijana.
HUDUMA NA MISAADA
 Kulipa karo na mahitaji muhimu kwa wanafunzi yatima walioko SekondariØ na vyuo mbalimbali. Kwa kipindi cha mwaka 2010 zaidi ya sh. 11,000,000/= zimetumika katika shuguli hii. Vikundi vingine 19 vilipata mkopo usiyo na riba kupitia mfuko wa microkrediti tangu mwaka 2009 hadi 2010.
 Wanawake 50 waishio na VVU/UKIMWI wamepewa msaada wa lishe.Ø
CHANGAMOTO
 Idadi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumuØ wanaohitaji msaada wa masomo  ni kubwa sana ukilinganisha na fedha ambazo kwa kiasi kikubwa zinazotolewa na wahisani kwa ajili ya kuwalipia gharama za masomo hivyo kutofikia malengo yaliyopangwa.
 Baadhi ya vikundi vilivyokopa kupita mfuko wa microcredit mwaka 2009Ø havijarejesha na hivyo kufanya kiasi cha deni kuwa shilingi 2,545,272.45/=
KUTOA ELIMU
Mafunzo ya ujasiliamali
Vikundi mbalimbali vya ujasiliamali vimekuwa vikipata elimu hususani kabla ya kuanzisha vikundi. Jumla ya Wanawake 55 waishio na UVV/UKIMWI wamepewa mafunzo ya ujasiliamali na kuhamasisha  waanzishe vikundi kwa ajili ya kupatiwa mikopo, mafunzo haya yalitolewa mwaka 2010.
CHANGAMOTO
 Baadhi ya vikundi vinahitaji zaidi ruzuku kuliko mikopo kwa sababu yaØ kutokujiamini katika shughuli zao hivyo wanahofia hasara ambayo inaweza kusababisha kushindwa kurejesha kwa wakati.
Elimu ya UKIMWI
Elimu ya UKIMWI imekuwa ikitolewa katika jamii kwa mfano kipindi cha mwaka 2010 elimu hii imetolewa kwa Watumishi 40 wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba  namna ya kujikinga na VVU, kuepuka maambukizi mapya na maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
CHANGAMOTO
Unyanyapaa bado ni tatizo katika utekelezaji wa shughuli za UKIMWI kwa sababu waathirika wengi bado hawajajiweka wazi na hili linaweza kuchochea maambukizi mapya.

Mchango wa KKKT Dayosisi ya Karagwe katika maendeleo ya jamii.

Askofu wa Dayosisi ya Karagwe Mh.  Dr. Benson Bagonza akiwa na wageni walioitembelea dayosisi toka Sweden mapema mwaka 2011 (Picha na Mchg.Oscar Samwel).
Dayosisi ya Karagwe ni miongoni mwa dayosisi ishirini zinazounda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Dayosisi ya Karagwe ilizinduliwa
rasmi tarehe 7/1/1979 pale Lukajange.

Tangu wakati huo dayosisi ya Karagwe imeendelea kujihusisha na maisha ya jamii ya wana Karagwe kwa kutoa huduma za kijamii na kuendesha shughuli za maendeleo katika wilaya za Karagwe na Ngara. Huduma zote zinazotolewa na Dayosisi ya Karagwe huwalenga wanajamii wote bila kujali dini zao, kabila wala rangi zao.
Zifuatazo ni huduma za maendeleo ambazo hutolewa na Dayosisi ya Karagwe.
1. Huduma za Afya- Dayosisi ya Karagwe inamiliki Hospitali ya Nyakahanga ambayo ndiyo hospitali teule ya wilaya ya Karagwe.Hospitali hii ni mkombozi kwa jamii ya watu wa Karagwe na maeneo jirani kama wilaya mpya ya Misenye. Huduma za kinga na tiba hutolewa katika hospitali hii.Pia hutoa huduma nyingine kama huduma ya afya ya msingi, upimaji wa virusi vya Ukimwi kwa hiari (ANGAZA), kliniki kwa ajili ya akina mama waja wazito nk. Pia hospitali ya Nyakahanga inaendesha na kusimamia zahanati nyingine nne ambazo ni Nyakatera, Ibamba-Mabira, zahanati ya shule ya sekondari Karagwe na Katenga-Ngara.
2. Mradi wa kudhibiti Ukimwi- Kutokana na janga la ugonjwa wa Ukimwi unaowatesa watu wengi, dayosisi ya Karagwe iliamua kuanzisha mradi huu ili kuwasaidia watu katika jamii ya Karagwe kwa kuwapatia elimu juu Ukimwi, kusaidia yatima hasa kuwalipia karo na mahitaji mengine kwa kusaidiana na familia, kutoa chakula kwa wanaoishi na VVU pamoja na mambo ya haki na utetezi hasa kwa wajane ambao kwa njia moja au nyingine huwa katika hatari ya kukosa haki zao katika familia za waume zao.


        Kilimo cha umwagiliaji Ihembe (Picha na Mchg.Oscar Samwel
3. Udiakonia na utetezi-Dayosisi ya Karagwe inawajibika katika kufanya shughuli za diakonia ikiwa ni kuwasaidia wasijiweza au watu ambao wanaishi katika mazingira hatarishi. Hapa makundi ya watu kama wazee, walemavu, wenye mtindio wa akili, nk husaidiwa katika kupatiwa mahitaji ya lazima ikiwemo chakula, mavazi, kuwajengea nyumba, kuwanunulia mashamba na kuwatetea wale walio katika hatari ya kukosa haki zao.Vilevile kitengo cha diakonia hutoa msaada wa mbuzi watano kwa kila familia iliyobainishwa kuwa maskini ili kwa njia hiyo mradi huo wa mbuzi uwasaidie kuongeza kipato cha familia ili waweze kujipatia mahitaji ya msingi pale nyumbani.  Pia kitengo hiki cha diakonia hutoa elimu kwa jamii ili ione umuhimu na wajibu katika kuwasaidia wenye shida maana wanaishi nao katia jamii moja.
4. Elimu- Hii pia ni sehemu muhimu ya kazi ya dayosisi ya Karagwe. Mpaka sasa dayosisi ya Karagwe inamiliki shule mbili za Sekondari ambazo ni Shule ya Sekondari Karagwe (KARASECO) na Shule ya Sekondari ya wasichana Bweranyamge. Katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2010 KARASECO imeshika nafasi ya pili (2) kimkoa kati ya shule 155 zenye idadi ya wanafunzi zaidi ya arobaini na ya 44 kitaifa kati ya shule 3196. Bweranyange imeshika nafasi 4 kimkoa kati ya shule 32 zenye wanafunzi chini ya 40 na ya 64 kitaifa kati ya shule 490. Pia dayosisi inamiliki shule mbili za kiingereza ambazo ni Tegemeo (English Medium) na Imani (English Medium). Vituo vingine vya elimu ni kama ifuatavyo: Chuo cha Biblia Nkwenda, Chuo cha ufundi na kilimo Nkwenda, Chuo cha ufundi staid kwa watoto yatima Lukajange, Chuo cha udiakonia na waalimu wa shule za awali Nkwenda. Pia katika upande wa elimu,dayosisi ya Karagwe inao mpango maalumu wa kuanzisha chuo kikuu hapa Karagwe na mipango inaendelea vizuri kwa matumaini kwamba chuo hiki kitaweza kuanza kupokea wanafunzi mwaka 2013 kama mipango yote itaenda kama ilivyopangwa.Ikumbukwe kwamba huduma zote za elimu hutolewa kwa watu wote bila kujali dini wala kabila.
5. Miradi ya Maendeleo: Dayosisi pia inasimamia miradi ya maendeleo kwa ajili ya jamii ya Karagwe na watu wengine wote kama ifuatavyo:Karagwe Hotel and guest house: Hiki ni kituo ambacho hutoa huduma za malazi chakula na ukumbi wa mikutano. Watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi hufurahia kutumia kituo hiki kwa sababu ya huduma zake bora, uaminifu wa wahudumu na utulivu uliop sehemu hiyo. Unafuu wa bei pia huwavutia watumiaji maana bei zetu zinalenga huduma zaidi kuliko biashara.  Miradi mingine ni kama mashine za kusaga nafaka huko majimboni, miradi ya maji, upandaji miti, uwanja wa Ndege Ihanda, miradi ya wanawake ya kuinua kipato chao kama ufugaji wa kuku, ushonaji nk

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana BweranyangeDayosisi ya Karagwe (Picha na Mchg.Oscar Samwel
6. Mradi wa utunzaji wa mazingira: Dayosisi ya Karagwe iko mstari wa mbele katika kutunza mazingira kwa kuamini kwamba mazingira ni uhai. Mradi huu unahusisha majimbo yote, sharika na mitaa ambapo inasisitizwa kwamba maeneo yote ya Kanisa yapandwe miti. Kwa mfano: Mwaka 2011 katika majimbo ya Mabira, Murongo, Bweranyange na Kyerwa jumla ya miti 500.000 ilipandwa chini ya mradi huu ambao uliazishwa mwaka 2004. Katika harakati hizi za utunzaji mazingira, dayosisi ya Karagwe kwa kushirikiana na Jimbo rafiki huko Ujerumani imeanzisha mradi wa mazingira uitwao KAKAUMAKI (Kampeni Kabambe ya Utunzaji mazingira Kituntu). Mradi huu unatekelezwa katika Jimbo la Kituntu na kwa mwaka jana jumla ya miti 17,500 ilipandwa. Pia dayosisi ya Karagwe inahimiza vituo vyake vyote ikiwemo mashule na vituo vingine kuhakikisha wanapanda miti kwa wingi ambayo mbali na kutunza mazingira lakini pia huko mbele ya safari itakuwa kitegauchumi pindi itakapovunwa.
7. Mradi wa Maisha mapya (New life in Karagwe) Huu ni mradi ambao ulianzishwa mwaka 2006 na unalenga kuwawezesha wanajamii kubadili maisha yao toka hali duni ya kipato hadi kupata hali nzuri na kumudu kutunza familia zao. Mradi huu unahusika na kuwasaidia wakulima waweze kulima kwa kutumia mbinu za kisasa ambapo mkulima hupewa Ng’ombe mmoja jike ili pamoja na kupata maziwa lakini pia mkulima hupata mbolea kwa ajili ya shamba lake na hivyo kipato cha familia kuongezeka. Upande wa wanawake wajane wao hupewa mbuzi wa maziwa. Mpaka sasa jumla ya Ng’ombe 300 na mbuzi 100 tayari wamegawiwa kwa walengwa. Pia semina hutolewa kwa wakulima jinsi ya kulima kwa tija na kutunza mazingira. Wakulima hupata nafasi ya kutembelea maeneo ya kilimo ili kujifunza kwa vitendo.Mfano mwaka 2010 wakulima walitembelea Maruku Bukoba na Igabiro ambapo walipata nafasi ya kujifunza kwa vitendo. Kadhalika mradi huu unawaelimisha watu juu ya utunzaji mazingira


8. Mradi wa kujengea uwezo watoto wa kike (wasichana): Mradi huu ni kwa ajili ya kuwasaidia wasichana walio katika umri mdogo vijijini na hata mashuleni ili waweze kujitambua na kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, ubakaji nk. Pia hufundishwa na kuelekezwa juu ya haki zao za msingi ili waweze kujitetea mbele ya jamii. Mbali na hayo pia mradi huu unalenga kuwabaini wasichana ambao kwa sababu za umaskini wa familia zao wameshindwa kuingia sekondari kwa kukosa karo. Wakishabainiwa mradi unawasaidia kuwalipia karo na mahitaji ya shule, mpango huu utaanza rasmi mwaka huu.
9. SACCOS: Huu ni mpango wa kuwasaidia wananchi ili waweze kuweka na kukopa kupitia vikundi vyao vya SACCOS ambao ulianza rasmi mwaka 2009. Mpaka sasa jumla ya Saccos 8 tayari zimesajiliwa katika majimbo ya Ihembe na Bweranyange. Kitengo cha Saccos ambaocho kiko makao makuu ya dayosisi Lukajange huwasaidia wanachama kuwapatia elimu kwa njia ya semina, kuwapa vitendea kazi hasa wakati wa kuanza kama vitabu, kasiki, nk. Pia kwa sasa wako katika kuziwezesha Saccos hizo kujenga ofisi za kuduma ambapo kikundi husaidiwa kupewa mabati, sementi, milango na madirisha ya chuma,vifaa vingine ni mchango wa wanachama.

Imeandaliwa na Mchg. Oscar S. Samwel





Baadhi ya habari zilizoko kwenye maktaba yangu ambazo ninataka niwajulishe au kuwarejesha kidogo ktk Karagwe yetu tunayoipenda tegemea nyingine zilizo current haswa upande wa elimu ambao tuko nyuma hatu kidato cha tano na sita kwa shule za serikali hii ni hatari nitawajuza tutakuwa na mjadala wa pamoja.

No comments:

Post a Comment